MWANAFUNZI
wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya St. Anthony Mbagala,
mkoani Dar es Salaam, Franco Donald Kisongo (18), amepotea jijini humo.
Shangazi
wa kijana huyo, Adelaide Kisongo amesema, Franco ni mgeni jijini Dar es
Salaam amepotea tangu Jumapili asubuhi ikiwa ni siku nne tu tangu
ajiunge na shule hiyo kuanza masomo ya kidato cha tano.
Kwa
mujibu wa Adelaide, kijana huyo aliwaaga wanafunzi wenzake kuwa alikuwa
anakwenda kwa shangazi yake Kariakoo, hakufika huko, na pia hakurudi
shule na hadi sasa haijulikani alipo.
Amesema,
walimu na walezi wa kijana huyo Mrangi, wametoa taarifa katika vituo
vya Polisi Mbagala Kizuiani, Chang’ombe na Msimbazi, na wanatumia RB
namba 3343/2012 ya kituo cha Msimbazi kumtafuta.
Kwa
yeyote mwenye taarifa kuhusu mahali alipo kijana huyo anaombwa kutoa
taarifa kituo chochote cha polisi au kuwasiliana na wenye namba
zifuatazo za simu. 0784- 384035, 0717-371763, 0713- 761006, na 0715- 247544





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)