AFYA YA KAMANDA GULUMO INAENDELEA VIZURI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

AFYA YA KAMANDA GULUMO INAENDELEA VIZURI

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=3530edf2ab&view=att&th=1362fc95b548c3da&attid=0.1&disp=inline&realattid=3a43467d63162072_0.1&safe=1&zw&saduie=AG9B_P-pMeAX8Bj6uum_JO85Z8o9&sadet=1332246867123&sads=4xNIXE0GPxBmY9Nl3SAUoZVOXyI 
 Msanii Mkongwe wa bendi Kongwe ya Msondo Ngoma Music,Muhidini Gurumo akiwa katika hospital ya Taifa Muhimbili, Dar es salaam jana, akipimwa mapigo ya Moyo na Ofisa Muuguzi Msaidizi wa Hospital hiyo,Suraiya Mohamed alipolazwa kufanyiwa uchunguzi wa kina toka mwishoni mwa wiki iliyopita.(Picha na www.burudan.blogspot.com)

Na Mwandishi Wetu


MWANAMUZIKI maarufu wa bendi kongwe ya  Msondo ngoma, Muhidin Gurumo aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ugojwa wa shinikizo la damu anaendelea vizuri.

Akizungumza na Dar es Salaam jana,Msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super 'D' alisema Afya ya  Gurumo inaendelea vizuri na wakati wowote anaweza kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo.

Alisema kuwa madaktari wanataka kuchukua vipimo vya mwisho kwa kina kujua kila kitu kinachop msumbua  katika mwili wake.


"Kwa sasa tunashukuru Mungu afya ya Gurumo inaendelea vizuri tofauti na mara ya kwanza na akiendelea hivi anaweza hakurusiwa hivi karibuni"alisema Super D.


Hata hivyo aliwataka wapenzi wa bendi hiyo kumuombea duwa mwanamziki huyo ili apone upesi pia aliongeza kwa kusema maonesho yao ya wikii hii ni kama ifuatavyo Alhamisi watakuwa Mwandege Mkoa wa Pwani,Ijumaa watapiga katika viwanja vya Lidaz Clab jumamosi watakuwa katika viwanja vya TCC Sigara na Jumapili watamaliza wiki endi katika ukumbi wa Max Bar uliopo Ilala Bungoni alisema Super D.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages