Mkuu
Mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Samwel Ndomba akila
kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikweteikulu jijini Dar es Salaam
leo asubuhi.Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi yaMeja Jenerali Samwel
Kitundu aliyestaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria.
Amiri
Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi miongozo ya kazi
mkuu mpya wa JKT meja Jenerali Samwel Ndombawakati wa hafla ya
kumuapisha iliyofanyika leo asubuhi ikulu jijini Dar esSalaam.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,(kushoto)Waziri Mkuu Mizengo Pinda(kulia) na
Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba wakiwakatika picha ya
pamoja muda mfupi baada ya hafla ya kumuapisha mkuu huyo mpyawa JKT
ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Amiri
Jeshi mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Katikati) akiwa katika picha
ya Pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis
Mwamunyange(kushoto) na Mkuu mpya wa JKT Meja Jenerali Samwel Ndomba muda
mfupi baada ya hafla ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es
Salaam leo
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mzeeAlbert Ndomba(85),baba
mzazi wa Mkuu Mpya wa JKT, Meja Jenerali Samwel Ndomba(wapili kushoto)
baada ya halfa ya kumuapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar es
Salaam leo.Kulia ni mke wa Meja Jenerali Ndomba na waliosimama nyuma ni
wanafamilia.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)