Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akizungumza kwa kusisitiza wakati wa mkutano wake na Walimu wa Shule ya
Sekondari ya Engutoto,Wilayani Monduli kuhusiana na hali ya elimu katika
shule hiyo kutoridhisha na kupelekea wanafunzi wengi wa shule hiyo
kufeli kwenye mtihani wa taifa wa kidato cha nne.Mkutano huo umefanyika
leo shuleni hapo,ambapo walimu wa shule hiyo walitoa changamoto mbali
mbali wanazomabiliana nazo.Mh. Lowassa amewaasa walimu wa Shule hiyo
kuwa wafanye kazi kwa juhudi ili kuwaandaa vijana wa taifa la
baadae.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo,Bw. Joseph Lukumay.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Shule ya Sekondari ya Engutoto,Bw. Joseph
Lukumay akitoa maelezo mafupi na kuwataka walimu wa shule hiyo kuanza
kuzungumzia ni kwanini shule yao imefanya vibaya kwenye mtihani wa taifa
wa kidato cha nne.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Shule ya Sekondari ya Engutoto iliyopo
Wilayani Monduli Mkoani Arusha,Mwl. Ally Muyago akitia taarifa fupi ya
shule yake kwa Mh. Edward Lowassa ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo la
Monduli,wakati wa mkutano wake na Walimu wa Shule hiyo kuhusiana na hali
ya elimu katika shule hiyo
kutoridhisha na kupelekea wanafunzi wengi wa shule hiyo kufeli kwenye
mtihani wa taifa wa kidato cha nne
Afisa Elimu Wilaya ya Monduli,Bw. Shaaban Mngunye (kushoto) akifafanua
jambo wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunde wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward
Lowassa kabla ya kuanza kwa mkutano na Walimu wa Shule ya Sekondari ya
Engutoto iliyopo Wilayani humo.
Walimu wa Shule ya Engutoto iliyopo Wilayani Monduli Mkoani
Arusha,wakizungumzia changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo katika
kazi yao ambapo wengi wamedai kuwa inachangia kwa kiasi fulani kudhorota
kwa elimu katika shule hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimsikiliza kwa makini,Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Shule ya
Sekondari ya Engutoto,Bw. Joseph Lukumay.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)