Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba (kushoto)
akiongea jambo na Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko huo Eugen Mikongoti
wakati wa mkutano kati yao na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Mfuko huo utatimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake tarehe 19 mwezi huu ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe zitakazofanyika makao makuu ya Bima ya Afya.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Emmanuel Humba (kushoto)
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mfuko huo
kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake tarehe 19 mwezi huu ambapo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa
Fedha , Mipango na Uwekezaji Deusdedit Rutazah akifuatiwa na Eugen
Mikongoti ambaye ni Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko huo.
Mkurugenzi Mwezeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Eugen Mikongoti akijibu maswali ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 ambapo waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
sherehe zitakazofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu Emmanuel Humba na kulia ni Mkurugenzi wa Fedha, Mipango na
uwekezaji Deusdedit Rutazah.
Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya Emmanuel Humba wakati wa mkutano kati yao uliofanyika leo
jijini Dar es Salaam kuhusu mfuko huo kutimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake mwaka 2001 ambapo waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zitakazofanyika tarehe 19 mwezi huu.Picha/Habari kwa hisani ya Full shangwe blogu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)