Kupambanisha
boxers zaidi ya mara tatu ni makosa kisheria, hapa kwetu tunafanya
kwa kutojua sheria au kwa mapromoter kutengeneza pesa. Wadau tumeliona
ilo na tukiendelea kukaa kimya tutalitia aibu Taifa.
International
fight zote zinaruhusu re-match na grand final after re-match, mfano
Manny Pacquiao vs Erick Morales game ya kwanza alipigwa Many paquiao
kwa points, akaomba re-match akashinda Manny Pac kwa KO round ya kumi.
Elick Morales akaomba grand final re-match akapigwa KO round ya 3,
akataka tena re-match sheria zikambana mpaka leo anataka kurudiana na
Manny Pac ila walishamaliza three times fighting.
Mfano
mwingine Manny Pacquiao vs Juan Manuel Marquez game ya kwanza draw,
ikaja re-match akashinda Manny pac kwa points, Marquez akaomba grand
final re-match ikapigwa akashinda Manny pac kwa pints ilikua very close
fight, mpaka leo wanataka re-match ila sheria za boxing zinawabana
haiwezekani tena.
Riddic
Bowe vs Evender Holifield zimepigwa three times, moja draw mbili
alipigwa Evander, na Evander alitaka re-match ikashindikana kwa kuwa
walishamaliza zile three times fighting na awawezi kupigana tena. Na
mifano mingi tu ila hiyo michache inatosha.
Hapa
kwetu tumeshuudia boxers wakipigana zaidi ya mara saba na watu kwa
kutojua sheria wanaona ni jambo la kawaida ila ni makosa kisheria, vyama
vyetu vya ngumi PST, TPBO, TPBC ect, baadhi vinajua hilo na baadhi
havijui hilo kabisa. Ni makosa kupiganisha watu zaidi ya mara tatu.
Rashid
Matumla vs Maneno Osward wamepigana zaidi ya mara 5 au 6 na bado
wanataka kupigana tena je hapo sheria zinafutwa au wanatubuluza?
Francis Cheka vs Rashid Matumla wameshapigana zaidi ya mara 4 na bado kuna plan ktk mwaka huu kuwapiganisha tena.
Mada
Maugo vs Francis cheka, walipigana PTA akapigwa Maugo, akaomba
re-match zikapigwa Morogoro Jamuhuri akapigwa tena Maugo, sasa
wameingia ktk grand final zitapigwa tena April tunaomba game hii iwe ya
mwisho kwao la sivyo tutawashtaki mapromoter na chama chochote
kitakachotoa kibali kwa ajiri ya fight nyingine baada ya hii ya April.
Mbwana
Matumla vs Francis Miyeyusho wameshapigana mara tatu wameshamaliza
ila wanataka kuandaliwa pambano la nne, je ni sheria zipi zinazofuatwa
hapo.
Vyama
vya ngumi za kulipwa walitazame hili kwa makini mkubwa sana tena
sana, kama sheria awazijui basi waulize au waingie ktk mitandao
waangalie na kufuatilia International fight na sheria zake, sio
kubuluza watu na huku wanafanya madudu.
Naomba kuwakilisha!
Mdau wa boxing






No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)