
Mamia
ya Wananchi wa Zanzibar kesho asubuhi wanatarajiwa kushiriki katika
mazishi ya aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la BUBUBU Marehemu Salum
Amour Mtondoo aliefariki Dunia leo katika Hospitali mkuu ya Mnazi
Mmoja Mjini Zanzibar baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kichwa.
Kwa
mujibu ya ratiba ya shughuli za Mazishi iliotolewa na Ofisi ya Makamo
wa Pili wa Rais Zanzibar imeeleza kuwa mnamo sasa tatu za asubuhi
maiti ya Marehemu itaondoka Mijini kuelekea Bumbwini Kijijuini kwao
kwa kusaliwa na baadae kuzikwa.
Katika
Mazishi hayo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed
Aboud atasoma risala na baadae Baraza la Wawakilishi Zanzibar itatoa
risala yake itakayosomwa na Spika wa Baraza hilo Pandu Ameir Kificho
na baadae Familia ya Marehemu Salum Amour Mtondoo itatowa tamko la
shukrani.
Tangu
Uchaguzi Mkuu Kumalizika wa Mwaka 2010 huyu atakuwa Mwakilisdhi wa
pili kufariki Dunia ambapo Mwakilishi wa kwanza kufariki ni
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini ambae pia alikuwa Mbunge aliechaguliwa na
Baraza la Wawakilishi Marehemu Mussa Khamis Silima wote hao wawaili
ni kutoka chama cha Mapinduzi.CREDITS: FATHER KIDEVU BLOG
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)