Mwili
wa Marehemu Tabu Bakari Mwangela (58), ukiwa umeharibika vibaya baada
ya kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika katika Kijiji
cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Ndugu wa marehemu wakilia baada ya kuuona mwili wake Tabu Bakari
Mwangela (58), aliyeuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu
wasiofahamika katika Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Waombolezaji
katika msiba wa marehemu Tabu Bakari Mwangela (58), aliyeuawa kwa
kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika katika Kijiji cha
Malamba wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
----
Watu
watatu wamefariki dunia mkoani Mbeya kwa matukio matatu tofauti
yaliyotokea Machi 7, mwaka huu likiwemo tukio la mtu kipigwa risasi,
kukatwakatwa na mapanga na jingine la kuchomwa kisu tumboni.
Tukio
la kwanza limetokea Kijiji cha Kongoro Mswisi, Kata ya Mswisi ambapo
mwananchi mmoja aitwaye Adam Jason Mwajeka (25), ameuawa kwa kupigwa
risasi tumboni na watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi Februari 7,
mwaka huu majira ya saa mbili usiku baada ya majambazi hao kuvamia
baadhi ya maduka na kupora pesa za mauzo katika maduka kadhaa.
Majambazi
hao waliokuwa na silaha walianza kwa kumzuia mwanamke anayefahamika kwa
jina la Tumpale Ally (32), ambaye ni mke wa Milele Kaponda kisha
kumpora pesa za mauzo shilingi milioni 2 za kitanzania, mita chache
kabla ya kuingia nyumbani kwake. Wakati wakibishana mwanamke huyo
alimuita mumewe na alipojaribu kutoka kumsaidia, majambazi hao
walifyatua risasi mbili hewani Tumpale aliachia pesa hizo kunusuru uhai
wake.
Haikuishia
hapo majambazi hao walivamia duka la Leonard Edwin Mwampyate (34), na
kupora pesa shilingi milioni tatu na laki tano, pamoja na simu ya
mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi elfu themanini na tano,
pia dukani alikuwepo nduguye Goliath Mwangonji ambaye walimwamuru kutoa
pesa kutoka mfukoni ambapo walimpora shilingi lakini mbili na elfu
ishirini.
Aidha
waliingia duka jingine linalomilikiwa na Bwaba Luka Mwasamaki na kupora
shilingi elfu sabini na walipokuwa wakitoka, walimfyatulia risasi Adam
Mwajeka tumboni na kufariki papohapo na katika harakati za kujiokoa
Elimu Konga (32), alipigwa risasi ya mguu na majambazi hao wakapata
nafasi ya kutokomea gizani.
Miongoni
mwa watu walionusurika katika tukio hilo ni pamoja na Diwani wa Kata
hiyo Bwana Furgence Mhegele na Askari wa usalama wa barabarani
aliyetayetambuliwa kwa jina moja la Salehe, na mazishi ya Adam
yamefanyika kijijini hapo huku Bwana Eliamu amelwanzwa katika Hospitali
ya Chimala Mission.
Tukio
la pili limetokea Kijiji cha Malamba wilaya ya Mbarali mkoani hapa,
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Tabu Bakari Mwangela (58)
ameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na mtu au watu wasiofahamika.
Mwili
wa marehemu umegunduliwa baada ya watu waliokuwa na ahadi ya kuuziana
shamba kumsubiri kwa muda mrefu shambani kwake, ndipo walipoamua
kumfuata nyumbani kwake na kukuta mlango ukiwa wazi, wakijua marehemu
hayupo mbali ndipo walipomuuliza jirani yake aitwaye Devotha Jeremia, na
kudai hafahamu alipo.
Watu
hao waliamua kugonga dirisha bila mafanikio yoyote na ndipo waligusa
mwili wa marehemu kwa kwa kupitisha mkono dirishani na kuamua kumuita
nduguye aitwaye Matrida Matiya (59), alipoingia nadni alikuta marehemu
akiwa juu ya kitanda chake ndani ya chandarua na alipopenyeza mkono
alikutana na damu kwenye kiganja na ndipo alipogungua kuwa nduguye
kauawa.
Bi
Matrida alitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Balaza la Kata Bwana Peter
Elias Sankala, ambaye naye alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa Kijiji
Ngumbushe Mwalyego na kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Igurusi
ambao walifika eneo la tukio na kufanya uchunguzi wa mwili wa marehemu
kwa kumtumia Daktari na kuukabidhi kwa ndugu na mazishi kufanyika
kijijini hapo.
Hata
hivyi hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusika na matukio yote mawili na
Jeshi la Polisi bado linaendelea kufanya uchunguzi ili kuweza kuwabaini
wahusika.
Wakati
huohuo Mwakingili Mwakaji anashikiliwa na Jeshi la Polisi, baada ya
kutuhumiwa kusababisha kifo cha Elias Mwalyego (37), baada ya kumchoma
kisu tumboni na kufariki papo hapo katika Kijiji cha Itimba wilaya ya
Chunya mkoani Mbeya.
Chanzo
cha kifo hicho ni marehemu kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa kudai rediuo
yake aina ya Rising yenye thamni ya shilingi 16,000 za kitanzania, ndipo
mtuhumiwa aliingia ndani huku marehemu akidhani mtuhumiwa kaenda
kumchukulia redio yake badala yake alitoka na kisu na kumchoma marehemu
tumboni na kufariki.
Diwani wa Kata ya Itimba Bwana Michael Zanzi amesema marehemu amesafirishwa kuzikwa eneo la Mbalizi.
Kwa upande wa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi amethibisha matukio yote matatu.Credit HAKI NGOWI BLOG





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)