Mama Salma Kikwete Ashiriki Maadhimisho Ya Maulid Ya Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania(JUWAKITA)Mkoa Morogoro - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mama Salma Kikwete Ashiriki Maadhimisho Ya Maulid Ya Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania(JUWAKITA)Mkoa Morogoro

Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kiwete akisalimiana na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislamu Tanzania ( JUWAKITA) Mkoani Morogoro Machi 18.2012 alipohudhuria Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW). yalioandaliwa na jumiya hiyo ya JUWAKITA.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete (vazi jeupe) akisindikizwa na Mwenyekiti Taifa wa (JUWAKITA) Shamim Khan, (kushoto) ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Halima Dendegu (wapili kutoka kulia) na Katibu Tawala Mkoa Morogoro Mgeni Baruwani baada ya kumaliza sherehe ya Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) Machi 18,2012 katika Chuo Kikuu cha Kiislam- Morogoro.
Wanafunzi wa madrasa wamsikiliza mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akizungumza nao.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete akiongea na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) kwenye sherehe ya Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad( SAW) Machi 18,2012 katika Chuo Kikuu cha Kiislam- Morogoro,
Mke wa Rias na Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete(kulia) na Mwenyekiti Taifa wa JUWAKITA Mama Shamim Khan kwa pamoja wakifuatilia ratiba katika Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) katika Chuo cha Kiislam- Morogoro.Maadhimisho hao yameandaliwa na Jumuiya ya Wanawake wa Kiislam Tanzania (JUWAKITA) mkoa Morogoro,Machi 18 2012,Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages