Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiweka jiwe la msingi katika Jengo jipya la Machinjio lililojengwa
katika Kijiji cha Ngelewala mkoani Iringa wakati akimalizia ziara yake
katika mkoa huo jana Februari 29, 2012. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, C. Ishengoma.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Kilimo
na Mifugo wa Manispaa ya Mafinga, Augustino Nyenza, wakati akitoa
maelezo kuhusu jengo jipya la Machinjio lililojengwa katika Kijiji cha
Ngelewela mkoani Iringa, jana Februari 29, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya wachungaji wa mkoani Iringa, baada ya kumaliza
majumuisho ya ziara yake katika mkoa huo jana Februari 29, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Mbunge wa Jimbo la Iringa mjini, kupitia tiketi ya CHADEMA,
Mchungaji Peter Msigwa, wakati akiwa Uwanja wa Ndege wa mkoani Iringa
jana akirejea jijini Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara yake ya
mkoani humo.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)