Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afanya Ziara ya Ghafla Kukagua Ujenzi wa Barabara ya Mzambarautakao - Finya - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Afanya Ziara ya Ghafla Kukagua Ujenzi wa Barabara ya Mzambarautakao - Finya

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua shughuli za ujenzi wa Bara bara ya Mzambarautakau hadi Finya unaofanywa na Kampuni ya S.H Young kutoka Nchini Kenya.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifanya ziara ya ghafla kuangalia ujenzi wa Bara bara ya Mzambarautakau hadi Finya unaojenja na Kampuni ya S.H.Youngya Nchini Kenya. Kushoto ya Makamau ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi.
--
 
Viongozi wa Taasisi za Mawasiliano, Umeme, maji pamoja na Mikoa wameagizwa kukaa pamoja katika jitihada za kutafuta mbinu za kutatua tatizo linalopelekea kuchelewa kwa ujenzi wa Bara bara ya Wete hadi Gando.

Agizo hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akikagua Ujenzi wa Bara hiyo inayojengwa na Kampuni ya Mecco .
Balozi Seif alisema juhudi za haraka zinafaa chukuliwa mara moja ili kuona urasimu unaopelekea kukwamisha utekelezaji wa mradi huo unaondoka.

“ Wananchi wanachokihitaji ni bara bara kwa ajili ya kuendelesha kwa uhakika shughuli zao za za Maendeleo. Hivyo ni vyema taratibu za ujenzi zikazingatiwa ili kuepuka gharama zisizokuwa na msingi” Alisisitiza Balozi Seif.

Aliwataka watendaji wa Taasisi hizo kulipa umuhimu zaidi suala la fidia kwa walioathirika na Vipando pamoja na mali zao ili kupunguza malalamiko kwa Wananchi na kuondosha vikwazo kwa wajenzi.

Mapema Kiongozi wa Kampuni ya Ujenzi ya Mecco Bwana Mohd Bujeti alimueleza Balozi Seif kwamba kumekuwa na tatizo la muda mrefu la uondoshwaji wa baadhi ya nguzo za umeme ambazo zimo katika maeneo yatayopitishwa Bara bara hiyo.

Bwana Bujeti alisema hali hiyo sio tu kwamba inachelewesha utekelezaji wa mradi huo bali pia inaongeza gharama kwa Kampuni yake jambo ambalo litapelekea kuitia hasara.

Ujenzi wa Bara bara ya Wete hadi Gando unatekelezwa chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Badea kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akitembelea ujenzi wa Bara bara Mzambarautakau kupitia Pandani, Kipangani, Kangani hadi Finya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliipongeza Kampuni ya S.H Young yenye makao Makuu yake 

Nchini Kenya kwa hatua nzuri waliyofikia ya ujenzi wa Bara bara hiyo.
Balozi Seif alisema hatua waliyofikia inatia moyo na kuwapa matumaini ya haraka Wananchi wanaosubiri kutumia Bara bara hiyo ambayo ni muhimu kwa Maendeleo yao Kiuchumi na Mawasiliano.

Mhandisi wa Mradi huo wa ujenzi Bwana Japhet Makimbi alimueleza Balozi Seif kwamba ujenzi wa bara bara hiyo yenye upana wa Mita sita unatarajiwa kukamilika rasmi mwezi Machi mwaka 2013.

Shirika la Changamoto ya Milenia la Nchini Marekani ndilo linalogharamia ujenzi wa Bara bara hiyo ya Mzambarautakau hadi katika Kijiji cha Finya Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amemaliza ziara yake ya siku tatu Kisiwani Pemba kwa kukagua shughuli za Kiuchumi na Maendeleo ikiwemo pia Miradi ya Kijamii.

 Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages