
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akilifungua Jengo
jipya la Skuli ya Sekondari ya Chambani akiwamwishoni mwa ziara yake ya
siku tatu kukagua miradi ya kiuchumi na maendeleo Kisiwani Pemba.
Kushoto yake ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh.
Zahara Hamad. 

Makamu
wa Pili wa Rais wa Z anzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapongeza Wakulima
wa Bonde la Maziwapacha ambao hawapo pichani katika Kijiji cha Chambani
Wilaya ya Mkoani. Kushoto yake ni Afisa Mdhamini wa Wizara ya Kilimo na
Mali Asili Pemba Dr. Suleiman Sheikh pamoja na Baadhi ya Wataalamu wa
Wizara hiyo.

Mshauri
wa Ujenzi wa Mradi wa Matengenezo ya Skuli ya Sekondari ya Fidel Castro
Pemba kutoka Kampuni ya M.S. Rans Co. LTD Bwana Nassor Al-Miskri
akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi alipofika kutembelea Mradi huo. Kushoto ya Balozi Seif Ni Mkewe
Mama Asha Suleiman Iddi
----
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema mfumo
unaotumiwa na Wananchi wa Jimbo la Chambani Mkoani Pemba wa kujumuika
pamoja katika kutekeleza Miradi ya Maendeleo bila ya kuingiza Siasa
unafaa kupongezwa na wapenda Maendeleo Nchini.
Balozi
Seif ameeleza kufurahishwa na mfumo huo mara baada ya kulizindua Jengo
Jipya la Skuli ya Sekondari ya Chambani akiwa mwishoni mwa ziara yake ya
siku tatu kutembelea miradi ya kiuchumi na Maendeleo Kisiwani Pemba.
Alisema
mfumo huo unasaidia kuachana na Siasa kwenye masuala ya Maendeleo hasa
lile la Elimu ambalo ndio Dira kwa ufanisi wa Wanafunzi wao hapo
baadaye.
“ Achaneni na Siasa katika masuala ya Maendeleo hasa lile la Elimu”. Alisisitiza Balozi Seif.
Aliipongeza
Kamati ya Skuli ya Chambani kwa jitihada zake za kuwajengea mazingira
mazuri ya Kielimu Watoto wao na kuwataka kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa
Nyumba za Walimu ili kuwarahisisha Wanafunzi hao kuwa karibu na Walimu
wao kwa muda wote.
Balozi
Seif aliwaasa Wazazi kuachana na tabia ya kuwaozesha waume watoto wao
mapema kwani kufanya hivyo ni kuwavurugia hatma yao ya kimaisha hapo
baadaye.
“
Tumekuwa tukiishuhudia tabia hii ndani ya Jamii inayofanywa na baadhi
ya Wazazi kuwaozesha Watoto wao wakiwa wanaendelea na Masomo na wengine
wamebahatika kuwa na kipaji kinachowawezesha kufikia ngazi ya chuo
Kikuu”.Alifafanua Balozi Seif.
Katika
Risala yao Wananchi hao wa Jimbo la Chambani wameiomba Serikali Kuu
kufikiria njia za kusaidia kutatua changamoto wanazokabiliana nazo
Jimboni humo likiwemo lile la ubovu wa Bara bara.
Wananchi
hao walimueleza Balozi Seif kwamba ukosefu wa Bara bara ya uhakika
Kijijini humo unapelekea kuviza kwa harakati zao za kila siku za
maendeleo.
Akimkaribisha
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ,Naibu Waziri wa Elimu
na Mafunzo ya amali Mh. Zahara Hamad aliahidi kwamba Wizara hiyo
itajitahidi kuona Jengo lililomalizika kujengwa kwa nguvu za Wananchi wa
Jimbo hilo linakamilishwa kuezekwa na Wizara kama utaratibu
ulivyowekwa.
Mh.
Zahra aliwaeleza Walimu na Wanafunzi wa Skuli hiyo kwamba Wizara ya
Elimu imo katika jitihada za kushirikiana na wahisani kwa lengo la
kufanikisha Mradi wa Tanzania ishirini na moja { Tanzania Twenty First }
unaokusudiwa kuewawezesha Wanafunzi kujifunza Kompyuta na Walimu
kufundisha kwa Kompyuta.
Katika
hafla hiyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alihamasika na kuahidi kuchangia shilingi Milioni 2,000,000/- kwa ajili
ya uendelezaji wa Jengo jengine Jipya la Skuli hiyo na Shilingi
500,000/- kusaidia Kituo cha Maandalizi cha Skuli ya Chambani.
Mapema
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikagua
Ukulima wa Mpunga wa kutegemea Mvua katika Bonde la Maziwa pacha
Chambani na kuwapongeza Wakulima wa Bonde hilo kwa hatua zao za
kuimarisha Kilimo cha Mpunga.
Akisalimiana
na Wakulima wa Bonde hilo Balozi Seif alisema Serikali iko mbioni
katika kuelekeza nguvu zake kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa
kukamilisha miundo mbinu itakayofanikisha mpango huo.
Alisema
kilimo cha umwagiliaji kinamuwezesha Mkulima kuendeleza Kilimo hicho
katika misimu miwili kwa mwaka na kuwaongezea mapato mara mbili pamoja
na chakula cha uhakika.
Halkadhalika
Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif alikagua Maendeleo ya matengenezo
makubwa ya Skuli ya Sekondari ya Fidel Castrol unaofanywa na Kampuni ya
Ujenzi ya Kizalendo ya M.S. Rans Co. LTD.
Mshauri
wa Ujenzi wa Kampuni hiyo Bwana Nassor Al-Miskri alimueleza Balozi Seif
kwamba ujenzi huo utachelewa kukamilika kama ilivyopangwa kufuatia
mapendekezo mengine ya kuongezeka kwa baadhi ya Majengo katika Skuli
hiyo.
Matengenezo ya Ujenzi wa Skuli ya Sekondari Fidel Castrol yanatarajiwa kugharimu zaidi ya Shilingi Bilioni tatu.
Na
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)