Habari Ankal Michuzi na Wanalibeneke woote,
Ni Tumaini langu kuwa mu
Wazima,samahani sana kutumia Neno hili lakini Nadhani Mnachokifanya ni
UKATILI,USALITI na Kuwapiga Mateke Watanzania Ambao Kodi zao ndio
zimekupeni TAALUMA hiyo ambayo mnatumia Sasa Kwa MAKSUDI kuwaua
Watanzania.
Katika Majadiliano
yoyote Huwezi Kuingia na Kutaka YAKO TU ndio Yachukuliwe Kama ni hivyo
Hakuna HAJA YA MAJADILIANO,ukiingia na RIGIDITY kuwa Yangu yote
Yatimizwe huna haja ya kujadiliana basi na Huna NIA YA SULUHU,ukikubali
Majadiliano Lazima ukubali kuwa FLEXIBLE Ukubali WIN-win Situation
,You win a little and Loose a little,hiyo ndio Formula ya kufikia
Maafikiano ktk Majadiliano yoyote.
Hivi tukijenga
Precedent ya Watu kutumia Umuhimu wao KUBLACKMAIL serikali Nchi Hii
Itakwenda wapi?? Wataalam wanaojua Mfano kuendesha Mitambo ya
Umeme,Maji Wote wakiamua izimwe ili Matakwa yao yatimizwe??
Ninyi hizo Mashine
Mtazitumia??,Wanajeshi wanaolinda Mipaka yetu Maporini Mvua,Radi Zao??
Polisi?? Nk itakuwaje? Sisi ni kama Mwili wa Binadamu kila Kada kwa
Nafasi yake inao Umuhimu wake, ni Majukumu Yanapishana tu,Kuwa Daktari
Anaokoa Maisha ya Watu Kitabibu,Lakini Polisi Anaokoa Maisha ya
Madaktari kwa Kupambana na Majambazi nk.
Hili suala la "Kutukuza"
Taaluma Fulani Nadhani ndio limepelekea Haya Yote.
Sijaribu Kudharau Taaluma Yenu,inao Umuhimu wake kwa Nafasi yake Lakini
hata Zingine zinao Umuhimu bila Walimu wa Shule ya Msingi Msingalikuwa
hapa ,Wazungu husema "From Little Acorns a Oak Grows".
Mwalimu Nyerere aliwahi
Zungumza "Wasomi ktk Nchi Maskini ni sawa na Wanakijiji wamejifunga,ili
ukasome uje kuwatumikia,sasa ukishahitimu Elimu ile Unawakimbia kwenda
Tafuta Maslahi Mazuri zaidi,Huu ni USALITI".
Hali duni ya Mishahara,Sekta ya Afya haitokani na
Udhaifu wa kiutendaji wa hawa Mawaziri, bali uduni wa Kifedha wa Wizara
na Serikali ikilinganishwa na Mahitaji ht Ukimuweka Ulimboka,Mkopi
hamtafanya Miujiza, ktk Dunia ya tatu kote Sekta ya Afya ni Duni si
kwetu tu,hii ni kuongopea Wananchi kwa Sababu mnazozijua ninyi.
Waziri Nkya,Waziri
Mkuu walijaribu kuwaengage wakati wa Mgomo huo,mkawakwepa si mara moja
Mama Nkya tulimuona, sote Tuliwaona.
Sio serikali inayosababisha Watu wafe ni Ninyi ambao Mnaacha watu
Wanakata Roho wakati uwezo na vifaa vya Kuwasaidia mnavyo na mmekuwa
Mkivitumia Miaka yote leo mnasema hakuna jp ndio ni duni.
Hili Sisi Tutasahau Mwenyezi
Mungu kamwe hatolisahau,Kutumia Uchungu wa Vifo vya Watanzania wenzenu
Kama FIMBO YA KUILAZIMISHA SERIKALI KUTIMIZA MATAKWA YENU,kwenu ni Bora
Binadamu afe kuliko Kukosa Maslahi,Mtizamo wa Ajabu sana kwa TRAINED
DOCTOR. Mimi si Masihi
naweza kuwa Wrong lakini hata Cardinal Pengo juzi alizungumzia Kuwa na
"ROHO YA KIMUNGU" madaktari wale walioendelea kuhudumia Binadamu wenzao
wakati wa Mgomo.
Namala najua
Hutonipenda kwa Haya lakini Ukweli kama niuonavyo Lazima
usemwe,Mnachofanya ni UKATILI USIOMITHILIKA Historia itawahukumu.
Leo Mponda na Nkya Wajiuzulu,Kesho Wananchi Wakiandamana mfano
Mkopi anyang'anywe Leseni ya Udaktari ana Kibri,Dharau na Katili?
Serikali wakunyang'anye tu?





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)