Napenda
kuwaarifu kwamba TPBC imetoa kibali cha mapambano sita (6) ya ubingwa
wa taifa yatakayofanyika jijini Tanga tarehe 4/3/2012 siku ya jumapili
katika ukumbi wa Community Center. Promota wa mapambano haya ni Ally
Mwanzoa wa Mwanzoa Boxing Promotion ya jijini Tanga.
Taarifa
hiyo imetolewa na Onesmo Ngowi pichani ambaye ni Rais wa IBF/USBA kwa
upande wa Afrika katika taarifa yake aliyotuma kwa vyombo vya habari
Amesema
katika taarifa hiyo kuwa washindi wa pamabano haya ya taifa watapambana
na mabondia toka nchi za Kenya na Uganda kugombea ubingwa mpya wa “Jumuiya ya Madola wa Afrika ya Mashariki” unaotambuliwa na Bazara la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) ambapo Kamisheni za Ngumi za Tanzania (TPBC) Kenya (KPBC) na Uganda (UPBC).
Makao makuu ya CBC yapo jijini London, Uingereza la linajumuishwa na nchi zaidi ya 59 duniani zilizokuwa chini ya utawala wa Ufalme wa Uingereza.
Kamisheni hizi tatu za TPBC, KPBC na UPBC ni wanachama pekee wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) kutoka ukanda huu wa Afrika ya Mashariki.
Ubingwa wa Taifa:
1. J.J. Ngotiko Vs. Ibrahim Habibu - Bantamweight (10 rounds)
2. Jumanne Mohammed Vs. na Juma Mokiwa - Featherweight.(10 rounds)
3. Haji Juma Vs. Omari Saidi - Flyweight weight (10 rounds)
4. Athumani Boxer Vs. Lucas Michael - Lightweight ( 10 rounds)
5. Saidi Mundi Vs. Saimon Zablon - Super Featherweight ( 10 rounds)
6. Zeberi Kitandula Vs. Bakari Shendeka - Super bantam ( 10 rounds)
Mapambano ya utangulizi yasiyo ya ubingwa.
1. Alibaba Ramadhani Vs. Juma Kihio Light Middleweight (8 rounds)
2. Hassan Ngonyani Vs. Puguto Omari Super Flyweight 6 rounds)
3. Patric Kimweri Vs. Issa Omari (light flyweight 6 rounds)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)