Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Dk. Christina Ishengoma akipata maelezo kutoka kwa
mkurugenzi wa mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakati
alipotembelea katika banda la kampuni hiyo katika uzinduzi wa wiki ya
maji inayofanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa kuanzia leo
Machi 16 ambapo imeelezwa kwa yatafungwa na Mh Dk.Rais Jakaya Kikwete
Machi 22.
Kampuni ya bia ya Serengeti ndiyo wadhamini wakuu wa maonyesho hayo
yakiwa na kauli mbiu ya "Maji kwa usalama wa Chakula", katik picha katikati ni Meneja wa Mahusiano ya Umma Nandi Miwyombela.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Dk Christina Ishengoma akihutubia wakati wa iringa katika ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Mkuu
wa mkoa wa Iringa Mh. Dk Christina Ishengoma akikata utepe kuzindua
rasmi maonyesho ya wiki ya maji kwenye uwanja wa Samora Mkoani Iringa
leo, kushoto ni Amani Mafuru Kaimu Mkurugenzi wa maji vijijini Wizara ya
maji.
Kutoka
kushoto ni Elias Amani Afisa wa mauzo (SBL) Imani Lwinga Meneja
Mawasiliano (SBL) Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya
bia ya Serengeti SBL na Nandi Mwiyombela Meneja Mahusiano ya Jamii
wakiwa katika picha ya pamoja huku wakionyesha baadhi ya vinywaji
vinavyozalishwa na kampuni hiyo.







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)