Watoto
washule wakip[ita katika daraja la muda lililowekwa na vijana wa
Manzese katika Mto Iteba unaotenganisha Sinza na Manzese jijini Dar es
Salaam. Pem,beni ni ujenzi wa daraja la kudumu ulioanza kufanyika hivi
karibuni chini ya Kampuni ya Ujenzi ya KIMD kutoka Kibaha mkoani Pwani.
Meneja
Miradi wa KIMD Constructor, Onesmo Nathan akimwelezea jambo kuhusiana
na ujenzi wa daraja la watembea kwa Mguu la ITEBA linalounganisha Sinza
na Manzese jijini Dar es Salaam linalojengwa na kampuni hiyo KIMD kutoka
Mjini Kibaha mkoani Pwani. KIMD ni moja ya kampuni chache za Ujenzi
zinazomilikiwa na wazawa kwa 100% na imekuwa ikifanya kazi nyingi za
ujenzi wa barabara, mashule, na vituo vya afya katika maeneo mengi hasa
Mkoani Pwani.
wananchi wakipita katika daraja hilo la muda ambapo hutozwa fedha na vijana hao.
Muuza
gahawa nae akipita jirani na eneo hilo la ujenzi wa daraja jipya ambalo
linajengwa kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni.
Kwamujibu
wa Meneja Miradi wa KIMD, Onesmo Nathan anasema ujenzi wa daraja hilo
unataraji kuchukua majuma manne lakini pia itatokana na hali ya hewa
itakavyo kuwa maana eneo hilo hujaa maji mengi wakati wa mafuriko.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)