Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel M. Maige (MB) kwa
Mamlaka aliyonayo amewateua wajumbe watano kuunda Bodi ya Wakurugenzi
ya Bodi ya Utalii (TTB) kuanzia tarehe 23 Machi, 2012.
Uteuzi huo unafuatia Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete kumteua Balozi Charles A. Sanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTB mapema wiki hii. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi hiyo itakayodumu kwa miaka mitatu ni pamoja na:-
- Prof. Isaya Jairo PhD, Mhadhiri wa Biashara na Uchumi, Chuo cha Usimamizi wa Fedha, IFM;
- Ndugu Teddy Mapunda, Mtaalamu wa Masoko (Marketing) na Afisa Uhusiano Serengeti Breweries Limited;
- Ndugu Samwel D.I. Diah, Mtaalamu na Mdau wa Biashara na Utalii na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Tanzania Travel Co. Limited;
- Mhe. Kaika S. Telele (Mb), Mbunge wa Ngorongoro na Mdau wa Utalii na;
- Mhe. Abdulkarim Shah (Mb), Mbunge wa Mafia na Mdau wa Utalii.
Habari na picha ni kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Maliasili na Utalii.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)