
Mchekeshaji
wa maarufu nchini kutoka kundi la Vuvuzela Entertainment, Evans Bukuku
akitoa maelezo machache juu ya kipindi chao cha Evans Bukuku's Comedy
Club kilichozinduliwa jana usiku, katika mgahawa wa Nyumbani Lounge
jijini Dar es Salaam. Kipindi kilichozinduliwa kwa kuonyeshwa Clouds TV
kitakuwa kikionyeshwa kila Jumatatu kuanzia saa 3 usiku na marudio yake
yatakuwa kila Jumamosi saa 8mchana.
Mchekeshaji wa maarufu nchini kutoka kundi la Vuvuzela Entertainment, Evans Bukuku akiwa pamoja na wageni wake.
Wageni walialikwa kutoka Clouds Fm&Tv Wasiwasi Mwabulambo, Arnold Kayanda, Abuu.
Ilikuwa ni full uhondo kwa hao wachekeshaji wenyewe
Mchekeshaji
wa maarufu nchini kutoka kundi la Vuvuzela Entertainment, Evans Bukuku
akiwatambulisha wachekeshaji wenzake wanaounda kundi hilo katika
uzinduzi wa kipindi uliofanyika Nyumbani Lounge, jijini Dar es Salaam.
Evans akionyesha vitu vyake.
Kiongozi
wa kundi la Vuvuzela Entertainment, Jacob Mwakamele akielezea machache
mbele ya wageni waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo. Picha zote na
Cathbert Kajuna wa www.kajunason.blogspot.com





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)