BREAKING NEWS: BWENI LA WASICHANA LA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM TAWI LA IRINGA (MKWAWA) LATEKETEA KWA MOTO - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

BREAKING NEWS: BWENI LA WASICHANA LA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM TAWI LA IRINGA (MKWAWA) LATEKETEA KWA MOTO

Kikosi cha Zimamoto na polisi wwakizima moto katika bweni la wasichana chuo cha Mkwawa mchana huu
Baadhi ya wanafunzi wakichukuliwa maelezo baada ya tukio hilo
Mali za wanafunzi zikiwa zimeteketea kwa moto 
Moto mkubwa ambao chanzo chake bado kufahamika umeteketeza vyumba viwili vya bweni la wasichana maarufu kama Hall 6 vyumba Block W katika chuo kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (MUCE) Iringa . Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa chanzo cha moto huo bado hakifahamiki . Walisema kuwa moto huo ulianza kuwaka katika chumba kimoja wapo chumba Block W muda wa saa 6 mchana na kuwa wakati huo baadhi ya wanafunzi walikuwa wamejipumzisha katika vyumba hivyo . Hivyo walisema kuwa waliona moto huo ukianza kuwaka katika chumba kimoja wapo na kuanza jitihada za kujaribu kuzima moto huo bila mafanikio hadi kikosi cha zimatomo kutoka Manispaa ya Iringa na jeshi la polisi walipofika kuzima moto huo. Mkuu wa chuo hicho cha Mkwawa Prof. Philimon Mushi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la moto japo amesema kwa sasa ni mapema sana kuelezea kwa kina suala hilo na kuwa taarifa zaidi ataitoa baada ya uchunguzi wa tukio hilo kufahamika ikiwa ni pamoja na kujua madhara yaliyojitokeza na chanzo cha moto huo. Uchunguzi wa mtandao huu umebaini kuwa moto huo umeanza kuwaka katika moja kati ya soketi za umeme katika chumba hicho hali inayoonyesha kuwa yawezekana watumiaji wa chumba hicho walikuwa wakitumia hita ama pasi 
 
Kwa Habari zaidi bofya link hiyo:http://francisgodwin.blogspot.com/
 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages