Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel, Sam Elangalloor akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa
Airtel 3.75G hii leo jijini Dar es Salaa katika makao makuu ya Kampuni
hiyo.
Meneja Maendeleo wa Bidhaa wa Airtel, Salum Madati akifafanua juu ya bidhaa hiyo mpya iliyozinduliwa hii leo.
Beatrice
Singano Mallya ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasilianowa Airtel akizungumza
wakati wa uzinduzi huo hii leo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu Sam
Elangalloor.
Wanahabari waliohudhuria uzinduzi huo hii leo.
Wanahabari wa Clouds FM na Times FM wakinukuu sauti kupitia virusha sauti.
Jumanne 13 Machi 2011, Dar es Saalam–Airtel
Tanzania leo imepiga hatua kubwa katika kujenga na kukuza mtandao wa
technoloijia ya 3.75G Africa kwa kuzindua rasmi mtambo wa 3.75G nchini
Tanzania,ambapo Airtel itatoa huduma ya internet yenye ubora na kasi
zaidi kwa watumiaji wenye simu zenye uwezo wa kutumia internet wawapo
mahali popote.
Mkurungenzi
Mkuu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangalloor alieleza”
kukua kwa technolojia hii kutakuza ufanisi katika vyombo mbalimbali vya
mawasiliano (multimedia), kwa kuwa 3.75G itatoa internet yenye ubora na
kasi zaidi kwa kuwezesha wateja kufungua tovuti mbalimbali, kufanya
maongezi ya simu kwa njia ya video , kuangalia TV, kutuma na kupokea
barua pepe na pia kupata muziki kutoka kwenye tovuti kwa kutumia simu.
Teknolojia
ya 3.75G itatoa nafasi kwa wateja kupata mawasiliano ya data kwa njia
tofauti na ya pekee kabisa, ndio maana leo Airtel tunajisikia fahari
kuwa internet yetu ya 3.75G ni uvumbuzi na muendelezo wa mtandao
(platform) wetu ili kuwawezesha wateja wa Airtel wote nchini kupata
huduma ya internet au data yenye ubora wa hali ya juu pamoja na kasi
zaidi”
Tunafanya
ubunifu wa kuleta huduma zenye ubora zaidi katika mtandao kwa
kuzingatia kuwa sasaivi dunia inauhitaji mkubwa sana wa huduma za
kimtandao hasa kupitia simu ya mkononi
Ukirejea
takwimu zilizofanywa na kampuni ya McKinsey & Co.
Telecommunications zinaonyesha mpaka sasa kuna watumiaji wa simu za
mkononi wapatao milioni 400 Afrika, na kwamba bara la Afrika ni moja
kati ya soko linalokuwa kwa kasi zaidi huku soko la simu za mkononi
likiendelea kukua na kupanuka zaidi na kufikia kutoa huduma za internet,
huduma za benki kwa njia simu (mobile banking) na biashara kwa njia ya mtandao yaani (mobile commerce) .
Hivyo
basi kwa kuzingatia hili, ndio maana Airtel tunaendelea na mikakati
kama hii ya kuwaletea wateja internet yenye kasi zaidi ya 3.75G ambayo
ni sambamba na lengo letu la kuendea kupanua mtandao ili kutoa mwanya
wa mawasiliano kuwafikia wakazi wengi wa vijijini ambao walikuwa
wamesahaulika na mapinduzi ya mawasiliano katika bara la Afrika.
“wote
tunafahamu kuwa mawasiliano ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya jamii ya
sasa lakini bado kunachangamoto kubwa sana katika kupata huduma hii kwa
baadhi ya sehemu barani Africa.
Lakini
tukumbuke Mawasiliano ni haki ya msingi kwa kila mtu na si vinginevyo
hivyo kwa kupitia mtandao wa Airtel internet yenye kasi zaidi ya 3.75G
ninaamini tutaweza kuunganisha idadi kubwa ya watu kwa kukuza mahusiano
ndani na nje ya ya jamii zetu, kuendeleza na kuutangaza utamaduni wetu,
pamoja na kupanua wigo wa wale wanaofanya biashara kupitia mtandao wa
internet “ Aliongeza Elangalloor.
Ikiwa
tayari mteja ameunganishwa na teknologia ya 3.75G simu yake itaonyesha
3.75G, HSDPA, WCDMA or HSPA. Hii inategemeana na Aina ya simu aliyonayo
mtumiaji lakini kasi ya kuunganishwa ni yenye ubora zaidi.
Airtel
itaendelea kuwekeza kwenye huduma ya data katika soko lake lote huku
lengo likiwa ni kuwa mtandao mpana zaidi wa teknologia ya 3.75G katika
bara zima, na itaendelea kutoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya
watumiaji.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)