KAMPUNI ya
mawasiliano ya Vodacom leo imemkabidhi hundi mshindi wa zawadi ya
kitita cha Shilingi Milioni Kumi wa droo ya mwezi ya promosheni ya
M-PESA Bw Peter James Kilalo.
Kilalo
amekabidhiwa hundi hiyo leo jijini Dra es salaam na Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacoim Tanzania Bw. Rene Meza katika hafla fupi
iliyohudhuriwa pia na waandishi wa habari.
Akipokea
hundi yake Bw. Kilalo ambae ni Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama
Barabarani Kituo Kikuu cha Dar es salaam ameshukuru kw akuibuka mshindi
jambo ambalo amesema hakulitegemea.
"Kwa
kweli mimi ni mteja mzuri sana wa M-PESA lakini kweli sikutegemea
kwamba ningeibuka mshindi, ila sasa ninapopokea hundi hii naamini kwamba
nimeshinda na fedha hizi Milioni kumi ni zangu"Alibainisha Bw. Kilalo.
Alipoulizwa
namna alivyojipanga kutumia pesa hizo Bw Kialalo alijibu" Jamani mimi
ni masikini na sikuwahi kuota kwamba ipo siku nitashinda kiasi kikubwa
cha fedha namna hii hivyo jambo kubwa kwangu kwa wakati huu ni kwanza
kuacha akili yangu itulie kabisa ndio niamue niziwekeze wapi ili
zinikwamue kimaisha"Alisema"
Nina
mawazo kadhaa ya biashara ambayo nimekuwa nikiyawaza kama njia ya
kutafuta namna ya kujikwamua kimaisha hivyo hizi pesa nitazielekeza huko
ila baada ya akili yangu kwanza kutulia kutoka katika hali ya furaha
niliyonayo sasa.
Aliongeza mshindi
huyo ametumia pia fursa hiyo kuwashauri watanzania kutumia huduma ya
M-PESA kwa kuwa mbali na kwamba imerahisisha maisha katika utumaji na
upokeaji fedha mijini na vijijini bado wanaweza kuwa katika nafasi ya
kushinda kama yeyeAwali
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza amesema promosheni hiyo
imelenga kuwawezesha wateja wa M-PESA kubadili masiha kutokana na
wanavyotumia huduma hiyo.
"Promosheni
hii tulizindua mwezi uliopita tukilenga kuwawezesha wateja wetu
kujishindia zawadi za fedha taslimu, kiasi cha Shilingi Milioni 480
kinashindaniwa ambapo hadi sasa wateja zaidi ya 4,000 wameshajinyakulia
zaidi ya Shilingi Milioni 120" Alisema
Bw. ReneAmesemaVodacom
inatambua umuhimu wa huduma ya M-PESA katika maisha ya kila siku ya
wananchi na hivyo wakati wote imekuwepo mikakati imara ya kuiwezesha
huduma hiyo kuendelea kuwa bora zaidi,salama na ya kuaminika sokoni.
"Matumizi
ya huduma ya M-PESA hapa nchini yamekuwa yakiongezeka kwa kasi sana,
kiwango cha wananchi kutuma na kupokea pesa pamoja na kufanya malipo ya
bidhaa mbalimbali kupitia M-PESA ni kikubwa jambo ambalo linakuwa
rahisi zaidi kutokana na mtandao mpana tulionao wa mawakala wanaofikia
20,000 mijini na vijijini."
Aliongeza Bw RenePromosheni
hiyo itadumu kwa siku tisini kutoka Februari 13, 2012 hadi May 13,
2012. Mbali na kutoa mshindi mmoja wa shilingi milioni kumi kila mwezi
pia kila siku washindi mia moja hujishindia Shilingi 50,000 kila mmoja.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)