Akabidhi mikopo nafuu kwa vikundi tisa vya Mirerani· kupitia mradi wa MWEI
Na Mwandishi wetu.
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Bi.
Mwamvita Makamba amewataka wanawake wajasiriamali hususan wadogo
kutambua kuwa maendeleo ya biashara zao na hatimae hali zao za kiuchumi
kutategemea pamoja na mambo mengine namna wanavyotumia vizuri fursa za
uwezeshaji wanazotengenezewa.
Bi.
Mwamvita ametoa changamoto hiyo Wilayani Simanajiro, Mkoani Manyara
katika kijiji Cha Mirerani wakati akikabidhi mikopo isiyo na riba wala
dhamana yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni Tisa kwa vikundi tisa
vya akina mama iliyotolewas na mradi wa Vodacom wa kusaidia
wajasiriamali wadogo wanawake wa MWEI.
Bi.
Mwamvita amesema kadiri ambavyo wanawake watakuwa tayari kutumia vema
fursa wanazotengenezewa ikiwemo ya MWEI wanajiweka katika nafasi nzuri
ya kujiwezesha kiuchumi na kuondokana na dhana kwamba mwanamke ni kiumbe
tegemezi. “Wanawake
wenzangu leo Vodacom inapowakabidhi mikopo isiyo na riba wala dhamana
ni fursa adhimu sana kwenu, ni wajibu wenu kutumia vema fursa hii
kujiinua kama ilivyokuwa wajibu wa Vodacom kuwatafuta, kuwafikia na
kuwawezesha, kazi sasa ni kwenu”Alisema Bi. Mwamvita.
Bi.
Mwamvita amesema kumekuwepo na kilio kikubwa cha wanawake wajasiriamali
wadogo kutofikiwa kwa urahisi ama kukosa uwezo wa kukopesheka kutoka
taasisi za fedha, hivyo katika kutimiza azma ya kubadili maisha ya
watanzania Vodacom ilibuni mradi wa MWEI kutatua changamoto hiyo. “Ni
vigumu kupata taasisi itakayokukopesha mfnyabishara wa vitumbua, genge
mchuuzi wa samaki, msusi n.k tena bila riba wala dhamana na zaidi
kukupatia mafunzo ya ujasiriamali kwa gharama zake, Vodacom licha ya
kwamba biashara yetu ni huduma za simu imethubutu kubuni mradi wa mikopo
kwa kuwa inapenda kuona maisha ya watanzania wakiwemo akina mama
yanabadilika”Aliongeza Mwamvita Aidha
Bi. Mwamvita amewataka wanawake hao kuhakikisha mikopo waliyoichukua
inleta tija katika biashara zao hasa kuinua mitaji ili nao waweze
kusimama na kusaidia wanawake wengine.
“Kabla
ya kuwakibidhi mikopo hii tumewapatia mafunzo ya ujasiriamali ikiwemo
somo la utunzaji wa mahesabu ya biashara, tutumie elimu hiyo na mikopo
hii kujiimarisha ili kuinua sauti zetu kwenye jamii”Aliongeza Mwamvita
huku akisindikizwa na vigelegele vya furaha kutoka kwa akina mama. Mradi
wa MWEI ni mahsusi kwa ajili ya kusaidia akina mama nchini kama mchango
wa Vodacom kuunga mkono juhudi za kitaifa za kumwezesha kiuchumi
mwanamke wa kitanzania na unalenga hasa wanawake wenye biashara zenye
mitaji ya kati ya Sh. 5000 na 200,000. Bi.
Mwamvita amesema kuwa mradi wa MWEI umejiwekea lengo la kuwafikia
wanawake wengi zaidi hususan maeneo ya vijijini ambao pamoja na kujituma
katika bishara ndogondogo wanakabiliw ana uchache wa fursa za
uwezeshaji.
“Ni
hatua muhimu katika maisha yetu kama Vodacom kusaidia ujenzi wa ustawi
wa jamii hapa nchini, tuna namna nyingi ya kubadili maisha ya watanzania
kama dira yetu invyosema, MWEI ni namna mojawapo”. Alisema Mwamvita.
Wakizungumza
mara baada ya kukabidhiwa mikopo hiyo mbali na kuishukuru Vodacom,
wanufaika hao wameahidi kuitumia vizuri mikopo hiyo ili kutimiza malengo
ya kibiashara waliyonayo.“Wengi
wetu hapa ni wajasiriamali wadogo tunaojishughulisha na biashara za
ususi, mama lishe n.k changamoto kubwa tuliyokuwa tukikabiliana nayo ni
kuweza kufikiwa na mikopo nafuu, leo tunafuraha kuona tumepata mikopo
isiyo na riba hata shilingi moja” Alisema Johari Mwaselela Mmoja wa
viongozi wa Vikundi.
Amesema
kupitia vikundi vyao, watahakikisha wanafanya kazi kwa pamoja na
kuhimizana ili mikopo waliyopatiwa itoe tija ya kuinua mitaji yao,
wakuze faida sambamba na kusaidia kubadili hali zao za maisha. Tunawaomba
Vodacom kama mlivyotufikia sisi hapa kijijini muwafikie na wenzetu
wengine waliopo vijijini kama sisi na muwaokoe, kwa kweli wanawke bado
tupo nyuma, tunawashukuru sana MWEI.”Aliongeza Mamam Mwaselela.
Awali
Meneja wa Mradi wa MWEI Bi Mwamvua Mlangwa alisema hadi kufikia Januari
mwaka huu kiasi cha Shilingi 150 Milioni kimeshatolewa na kunufaisha
akina mama zaidi ya 6,000
Bi.
Mwamvua amesema idadi ya wanaohitaji mikopo hiyo ni kubwa hivyo
amewasihi kina mama hao wa Mirerani kutumia vizuri fursa hiyo na
kuhakikisha wanarudisha mikopo kwa wakati ili kuwafikia wanawake wa
sehemu nyengine nchini. Kupitia
mradi wa MWEI Vodacom huvipatia vikundi vya akina mama mikopo pamoja
na mafunzo ya ujasiriamali kazi ambayo hufanywa na Shirika la kuhudumia
viwanda Vidogo – SIDO kwa gharama za Vodacom. Mikoa
ya Arusha, Manyara, Morogoro, Tanga, Rukwa na Katavi, Dodoma, Mara,
Mwanza,Shinyanga na Pwani imeshanufaika na mikopo ya MWEI tangu mradi
huo ulipoanzishwa mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)