Waziri
Mkuu Mizengo Pinda (katikati) akitoa tamko la kuwataka baadhi ya
madaktari waliogoma kurudi kazini leo katika ukumbi wa mikutano wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakati alipokutana na kuzungumza na
madaktari na kutoa tamko la kuwasimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Mutasiwa.
Baadhi
madaktari wakifurahia Kauli iliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda katika mkutano wao na katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH) leo.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Madaktari, Steven Ulimboka akitoa tamko la kurejea kazini
kwa baadhi ya madaktari walioko katika mgomo kesho, mara baada ya
Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuondoka.
Baadhi
ya madaktari wakiwa katika mkutano wao wa kujadili kuhusu kurudi
kazini mara baada ya Waziri Mkuu Mizengo kuondoka katika ukumbi wa
mikutano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na madaktari leo baada ya kuwataka
kurejea kazini ili kuwahudumia Watanzania katika Ukumbi wa mkutano wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Watu mbalimbali wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati wa mkutano huo. Picha zote na Magreth Kinabo – MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)