Mshiriki wa shindano la “Cheza, Vaa, Imba Lama Rihanna” akionyesha uwezo wake wakati wa utambulisho wao.
“Rihanna” mwingine akionyesha uwezo wake.
...Akionyesha “machejo” yake.
Nameless akitumbuiza na mmoja wa mashabiki aliyemwita apande jukwaani.
Kiongozi wa Mashauzi Classic Band, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’, akinengua na mpiga gitaa wake.
...Akiwajibika jukwaani.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Zuhura, akipagawisha mashabiki.
Juma Nature akiongea na mashabiki wake.
Juma Nature “akipeana tano” na mashabiki wake kabla ya makamuzi.
Kundi zima la Wanaume Halisi likiwajibika jukwaani.
Mwanamuziki Ambwene Yesayah ‘AY’, akiwasalimia mashabiki.
Wasanii wa kundi la Wakali Dancers wakikamua wimbo wa Michael Jackson.
Wanamuziki wa bendi ya FM Academia wakiwajibika.
Kina “Rihanna” wakionyesha ujuzi wao.
sha Mashauzi akiwa kazini.
Wanenguaji wa FM Academia wakionyesha uwezo wa nyonga zao.
….Akina Rihanna Wakiwa kwenye pozi la pamoja.
Mashabiki waliofurika katika tamasha hilo wakifuatilia burudani hiyo.
Hali halisi ya umati ulioingia ukumbini hapo
--
MASHABIKI waliohudhuria burudani katika kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam walipata starehe ya kutosha kutoka kwa wanamuziki Juma Kassim ‘Sir Nature’ wa hapa nchini, na Namelesa kutoka Kenya ambapo walitoa makamuzi ya nguvu usiku wa kuamkia leo.
Wanamuziki hao walitoa kauli za kuushukuru umati mkubwa uliojitokeza kwenye onyesho hilo wakisema hawakutegemea Mbagala kuwa na mashabiki wa burudani wengi hivyo.
Shoo hiyo ilisindikizwa na Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Mashauzi Classic Band, Wakali Dancers, Zuhura na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya huku washiriki wa shindano la “Cheza, Vaa Imba Kama Rihanna” wakitambulishwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)