Mbunifu
wa mavazi mama Asia Idarous Khamsin (wa pili kulia) wa Fabak Fashion
ambaye pia ni muandaaji wa onyesho la Lady and Red 'Reloaded ' 2012
akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia
onyesho linalotarajiwa kufanyika Februari 10, 2011 katika hoteli ya
Serena jijini Dar es Salaam. Kulia ni Bw. Mauldi Mlawa ambaye ni Katibu
wa Kikundi cha Kikale Youth Care kilichipo wilayani Rufiji na Meneja wa
kinywaji cha Redds Original, Victoria Kimaro ambao ni wadhamini wakuu wa
onyesho hilo. Onyesho hilo linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu wapatao
30 ambao wataonyesha mavazi yao.
Meneja
wa kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro ambao ni wadhamini wakuu
wa onyesho hilo pembeni yake ni Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous
Khamsin wa Fabak Fashion ambaye pia ni muandaaji wa onyesho la Lady and
Red 'Reloaded ' 2012 pamoja na Bw. Mauldi Mlawa ambaye ni Katibu wa
Kikundi cha Kikale Youth Care kilichipo wilayani Rufiji. Onyesho hilo
linatarajiwa kuwakutanisha wabunifu wapatao 30 ambao wataonyesha mavazi
yao.
Katibu
wa Kikundi cha Kikale Youth Care kilichipo wilayani Rufiji Bw. Mauldi
Mlawa akifafanua jambo kuhusu kituo maalum cha kusaidia waathirka wa
dawa za kulenywa kiitwacho "Kikale Youth Care Group" kinachotarajiwa
kufunguliwa Rufiji ambapo Mbunifu wa mavazi mama Asia Idarous Khamsin wa
Fabak Fashion ambaye pia ni muandaaji wa onyesho la Lady and Red
'Reloaded ' 2012 atachangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo.
Kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro ambao
ni wadhamini wakuu wa onyesho hilo.
---
Onyesho
la mavazi lijulikanalo kwa jina la 'Lady in Red 2012' linaloandaliwa na
mama wa mitindo Tanzania Asia Isarous Khamsin ni la saba kwa mwaka huu.
Mama
Asia Idarous Khamsin atakuwa anatimiza maonyesho ya mavazi yapatayo 100
kwa Tanzania tu mbali na maonyesho mengine ambayo amefanya nchi za nje.
Hivi sasa mama wa mitindo anafanya kazi zake Tanzania na USA.
Mwaka huu onyesho hilo litazindua kituo maalum cha kusaidia waathirka wa dawa za kulenywa kiitwacho "Kikale Youth Care Group"
Wabunifu
wapatao 30 watapanda jukwaani siku hiyo kuonyesha miotindo tofauti ya
mavazi na tiketi zimeanza kuuzwa FABAK Fashions, Mikocheni Dar es Salaam
na kwa mawasiliano zaidi unaweza kupiga 0784263363.
Picha na Habari na C.A. Kajuna, Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)