Refa wa Kimataifa Nchini, Gratian Hemans Matovu Afariki Dunia - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Refa wa Kimataifa Nchini, Gratian Hemans Matovu Afariki Dunia

Aliyekuwa Refa wa Kimataifa hapa nchini, Gratian Hemans Matovu (pichani), amefariki dunia leo jijini Dar es Salaam.

Kwa kujibu wa taarifa zilizotufikia hivi punde, kutoka kwa mtoto wake Bw. Stephen Matovu, Mzee Matovu amefariki leo majira ya saa 6 mchana huko nyumbani kwake Mbezi Beach (Makonde) na taratibu za mazishi zinaendelea hapo hapo nyumbani kwake.

Mzee Gratian Matovu alianza kuwa refarii wa kimataifa tokea miaka ya 1964 na aliendelea na shughuli hiyo hadi miaka ya 1970 na hadi Mwaka 2006 alikuwa bado katika Kamati ya Marefarii Tanzania.

HISTORIA FUPI

Mzee Matovu alipata Diploma ya Urefarii kunako miaka ya 1956 na akaja kuwa refarii Daraja la Kwanza mnamo Mwaka 1961. Miaka Mitatu baadae alipata Beji ya FIFA.

Mzee Matovu alipata kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Chama cha Marefarii Tanzania.

Kwa Taaria zaidi za wasiliana na STEPHEN MATOVU 0713576666

Mungu Amlaze Mahala Pema Peponi Amina

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages