Mzee
wa Kimasai mkazi wa Longido akimshukuru na kumuombea dua njema Rais
Dr.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mzee huyo kukabidhiwa ng’ombe watano
na mbuzi watano wilayani Longido jana.Mzee huyo ni mmoja wa wafugaji
walipoteza mifugo yao yote kufuatia ukame mkali uliozikumba wilaya za
Longido,Ngorongoro naMonduli.
Mwanafunzi Godlisten Ole Olais
anayesoma kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Longido akiteta
jambo na Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete
kuwasili katika viwanja vya sekondari hiyo kuongoza uzinduzi wa wa mradi
wa serikali wa uwezeshaji mifugo(seed stock) kwa kaya za wafugaji
waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame msimu wa 2008-2009 na
2009-2010 zilizofanyika wilayani longido jumapili.







No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)