AMINI MWINYIMKUU - BONGO FLAVA ARTIST
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Amini, amesema kuwa ametimuliwa rasmi Tanzania House of Talents ‘THT’, lakini anahisi kama ameonewa kutokana na mabavu yaliyotumika.
Vyanzo vya habari vililipoti kuwa msanii huyo anajandiliwa na uongozi,
lakini sasa taarifa iliyopatikana kutoka kwa muhusika zinadai tayari
ameshawekwa pembeni.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,
huku akitokwa na machozi alisema kuwa uongozi haujatenda haki kwani
kosa la kinidhamu alilofanya walipaswa kukaa naye na kuzungumza
lakini wameamua kumfukuza kitu ambacho anahisi ameonewa.
“Mimi sioni kama kuwa wema ndani ya THT, ila nachoweza kusema kwamba
naenda kufanya muziki wangu na mungu atanijalia tu kwa sababu kila kitu
ni mipango,”
Amini alipigilia msumali wa mwisho.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)