TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Precision Air yafanya mabadiliko katika safari
zake Johannesburg
Dar es Salaam, Februari 24 2012. Precision Air- Shirika la ndege linaloongoza Tanzania leo
imetangaza kufanya mabadiliko katika ratiba yake ya safari kwenda Johannesburg,
ambapo itaanza kuondoka saa 11 jioni badala ya saa 2 kama hapo awali kwa ajili
yakuwezesha wasafiri wake kuweza kuwahi na kuwapatia urahisi wa kuunganisha
safari kwenda kwingine.
Akizungumza
katika makao makuu ya shirika hilo Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Biashara Bw.
Patrick Ndekana amesema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya utafiti uliofanywa
na shirika hilo, ambayo imependekeza kwamba watumizi wa huduma hiyo
wanapendelea kusafiri mapema kwa ajili ya kupata urahisi wa kuunganisha safari
kwenda kwingine, pamoja na kujihakikishia usalama kwa wanaoishia uwanja wa kimataifa
Oliver Tambo jijini Johannesburg.
“Kaunzia Februari tarehe 29 mwaka huu tutaanza
kuondoka Dar es Salaam saa 11 jioni na kufika jijini Johannesburg saa 1:45
usiku,” alisema Bw. Ndekana.
“Tunaamini
kwamba mabadiliko haya ya ratiba yatavutia idadi kubwa ya wasafiri pamoja na
kutuongezea biashara nzuri zaidi kwa shirika letu,” aliongeza.
Mkurugenzi
huyo pia alisema kwamba pamoja na kufanyika kwa mabadiliko hayo, muda wa kurejea
kutoka Johannesburg kuja Dar es Salaam hautabadilishwa. “Muda wa kutokea
Johannesburg utabakia pale pale saa 5:50 na kufika Dar es Salaam saa 10:20
alfajiri,” alisema.
Kwa
mujibu wa Bw. Ndekana mabadiliko hayo yanaashiria pia kwamba Precision Air wana
umakini wa kusikiliza na kuchukulia maanani mawazo mbali mbali kutoka kwa
wateja wake.
“Kama
shirika la umma iliyoorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam kupokea
maoni mbali mbali kutoka kwa wanahisa na wadau wetu ni jambo jema, ambayo
tunaamini kwamba inatuongezea thamani kubwa kama shirika la ndege,” alisema.
Wakati
huo huo, shirika hili ikishirikiana na shirika la ndege la Kenya Airways
imeweza kuongeza idadi ya safari za moja kwa moja baina ya Dar es Salaam na
Nairobi kutokea 4 hadi 5 kwa siku.
Akizungumzia
nyongeza hiyo Bw. Ndekana amesema kwamba safari hizo zitafanyika kwa
kushirikiana na Kenya Airways, ambao shirika hilo la Kenya litaratibu safari 2
wakitumia ndege aina ya Embraer 190 (E190) wakati Precision Air wakiratibu
safari 3 kutumia ndege yao ya B733.
“Jambo
la kuvutia katika hizi safari ni kwamba zote zitatumia ndege aina ya Jet, na
sio ATR’s, ambayo inamaanisha usafiri murua zaidi kwa wateja wetu maana
watatumia muda mfupi wakiwa angani,” alisema.
Safari
ya nyongeza ya Nairobi kutokea Dar es Salaam inatarajiwa kuanza sawia na
mabadilko ya safari ya Johannesburg, tarehe 29 Februari, 2012.
“Kuna
idadi kubwa ya wasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Nairobi, na kurudi – ambayo inajumuisha wafanyabiashara
na wafanyakazi wa makampuni kutoka sekta mbali mbali,” aliongeza Ndekana.
Shirika la ndege la
Precision Air ina mtandao mkubwa nchini kuliko mashirika yote Tanzania, ikiwa
inafanya safari kwenda; Dar es Salaam,
Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Bukoba, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga,
Mtwara. Kikanda Precision Air inasafiri kwenda
Nairobi, Mombasa, Entebbe, Hahaya na Johannesburg.
Mwisho.
Imetolewa na Ofisi ya
Mawasiliano. Tel: 0786 404 010/0712
223 839
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)