Wimbi
la wizi limeendelea kushamiri na kuchukua sura nyingne baada ya
waandishi wa habari wawatu mkoani Mbeya kuibiwa mali zao na vitendea
kazi.
Waandishi
wa habari waliokumbwa na mkasa huu ni pamoja na mwandishi wa gazeti
la Nipashe Bwana Thobias Mwanakatwe, mwandishi wetu wa mtandao Mbeya
Yetu Bwana Ezekiel Kamanga na mwandishi wa TBC Bwana Hosea Cheyo,
kituo cha Mbeya ambaye majira ya saa 9 kamili usiku, eneo la Iwambi
jijini Mbeya kuibiwa Desktop computer, Laptop mbili, TV inch 21,
Kamera aina ya Sony, External hard disk, chaji ya kameraBroadband wire
na Broadband Charger vyote vikiwa na thamani ya shilingi 3,620,000 na
watu wasiofahamika.
Mbinu
iliyotumika katika uporaji wa mali hizo ni kuvunja.kitasa cha mlango
na kisha kuingia ndani, na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea .
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Jeshi la polisi Advocate Nyombi amesema baada ya
msako mkali wamefanikiwa kuwakamata watu wawili katika kijiji cha
Mlowo wilayani Mbozi, wakati wakisafirisha mali hizo kwenye gari aina
ya Toyota Mark II lenye nambari za usajili T 952 ATR.
Watuhumiwa
hao waliokamatwa ni pamoja na Kiongozi wa wizi huo Bwana Filbert
Mbunda mkazi wa Mbalizi na dereva Christian Asajile, wakati mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Fadhili alikimbia, baada ya gari hilo
kusimamishwa na Polisi wakati likielekea Tunduma.
Hata
hivyo Bwana Hosea Cheyo amelishukuru jeshi la polisi kwa utendaji wao
wa kazi ipasavyo, kutokana na kuijali jamii kwa kuweza kutatua kero
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama.
Source-Mbeya yetu Blog.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)