Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Chuo cha VETA cha Shinyanga akiwa katika
ziara ya mkoa huo, Februari 26, 2012. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Ally Nasoro Rufunga.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mafunzo ya ushonaji wakati alipozindua
Chuo cha VETA cha Shinyanga akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari
26,2012.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mafunzo ya ukatibu muhtasi wakati
alipozindua Chuo cha VETA cha Shinyanga akiwa katika ziara ya mkoa huo
Februari 26, 2012 .
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kwenye
eneo la hospitali ya Iselamagazi kukagua ujenzi wa hospitali hiyo
iliyoko jimbo la Solwa na kuhutubia mkutano wa hadhara Februari 26,
2012. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga.
Msanii
wa ngoma ya asili ya Kisukuma (jina halikupatikana) akionyesha fiisi
wakati kikundi chake kilipotumbuiza katika mkutano wa hadhara
uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kijiji cha Chela
wilayani Kahama Februari 25, 2012
Mpiga
zeze wa Kijiji cha Iselamagazi katika jimbo la Solwa Shinyanga (jina
halikupatikana) akitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokagua
ujenzi wa hospitali na kuwahutubia wananchi wa kijiji hicho akiwa
katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 26, 2010
Mbunge
wa Solwa Ahmed Ali Salum (mwenye kaunda suti) akisakata zeze katika
mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye
eneo la hospitali ya Iselamagazi, Shinyanga Februari 26, 2012
Wasanii
wa ngoma ya Kisukuma ya Buyeyewakicheza ngoma hiyo wakati Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shycom
Mjini Shinyanga, Februari 26,2012.
Askari
wa Jadi yaani Sungunsu wa jimbo la Solwa wakicheza ngoma yao wakati
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokagua ujenzi wa hospitali ya Iselamagazi
na na kuhutubia mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya mkoa wa
Shinyanga Februari 26,2012.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)