Mtoto Cesilia Edward Afariki Dunia - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Mtoto Cesilia Edward Afariki Dunia


Cesilia Edward akiwa na Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamid Mtoto Abdulkarimenzi za uhai wake
--
Mtoto Cesilia Edward amefariki dunia saa tano usiku wa tarehe 08 katika hospitali ya Regency ya hapa jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amelazwa kwa siku mbili kwaajili ya matibabu
Marehemu Cesilia alikuwa na umri wa miaka 14 alikuwa na tatizo la moyo na figo kushindwa kufanya kazi na kusababisha tumbo kujaa maji na kuvimba aligundulika na tatizo hilo tangu alipozaliwa.
Kampuni ya Africa media Group wamiliki wa Channel ten Kupitia kipindi mimi na Tanzania ilifanikiwa kumpeleka marehem Cesilia nchini India kwa matibabu mwaka 2011 mwezi Oktoba lakini hakufanikiwa kupata matibabu (operation) baada ya madaktari kuthibitisha kuwa alikuwa amechelewa kwa matibabu.

Cesilia alikuwa mtoto ya tima na kulelewa na familia ya Bw. Peter Nyarugembe mkazi wa Mbagara kuu ambaye alikuwa akimlea baada ya kukuta akilelewa na dada yake wilayani Kisarawe na alimkuta na tatizo hilo ila kutokana na hali ya uchumi aliyo nayo hakuweza kumsaidia kupona ugonjwa alio nao na kuamua kuomba msaada kwa wasamalia wema kupitia Kipindi cha mimi na Tanzania.
Marehemu alifikishwa hospitali jumatatu ya tarehe 6 mwezi huu akiwa na hali mbaya iliopelekea kupoteza fahamu na kumbukumbu kila wakati hali iliendelea hivyo mpaka umauli ulipo mkuta Mungua ailaze roho ya marehemu Cesilia mahala pema peponi Amen.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages