Vijana
wa umoja wa waendeshaji mapikipiki wa chama cha Mapinduzi
wakimsindikiza mgombea wa Uwakilishi wa chama hicho junbo la Uzini
Mohamed Raza katika uzinduzi wa kampeni wa kuwania kiti cha Uwakilishi
Jimbo hilo hapo jana.
Kijana
wa chipukizi Zawadi Mbaraka akimvisha Skafu Makamo mwenyekiti wa CCM
Zanzibar Dk Amani Karume baada ya kuingia katika Uwanja wa Mkutano wa
CCM kwa ajili ya kuzindua kampeni ya chama hucho huko Uzini wilaya ya
kati Unguja.
Makamo
mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akibadilishana mawazo na
Makamo Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa huko katika kiwanja
cha mpira Uzini wakati wa kuzinduakampeni ya kugombea Uwakilishi wa
jimbo hilo.
Wananchi
mbalimbali pamoja na wakereketwa wa chama cha CCM wakiwa katika
mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika huko katika kiwanja cha
Uzini Zanzibar kwa ajili ya kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo
hilo ndugu Mohd Raza.
Makamo
mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akimnadi mgombea wa Kiti
cha Uwakilishi jimbo la Uzini ndugu Mohd Raza Huko katika kiwanja cha
Mpira Uzini hapo jana .
Mgombea
wa Uwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza akihutubia wananchi pamoja
na wanachama wa chama cha Mapinduzi baada ya kutambulishwa rasmi kwa
wanachama hao hapo jana Kuliani kwake ni Makamo mwenyekiti wa CCM
Zanzibar Amani Abeid Karume.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)