Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Patrick Ndekana akifurahia kumaliza mbio za Vodacom Fun Run.
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Bw. Patrick Ndekana akihojiwa na waandaaji wa Kili Marathon - Wild Frontiers.
...................
Kaimu Mkurugenzi wa Biashara
wa Shirika la ndege la Precision Air Bw. Patrick Ndekana ametoa wito kwa
watanzania kushiriki katika michezo na utalii wa ndani ili kuweza kushindana
kimataifa na kujenga utamaduni wa kuenzi urithi wetu.
Akizungumza mkoani
Moshi hivi karibuni kama mdhamini wa Kilimanjaro Marathon, Ndekana alisema,
“Tanzania ina vipaji vingi sana katika michezo, ikiwemo riadha. Naamini kabisa
kwamba wadau tukijipanga vizuri tutaweza kuibua majina makubwa wa michezo
kutoka taifa hili.”
“Kwa kutambua umuhimu
huu ndo maana sisi kama Precision Air tumeweza kudhamini riadha hizi kama
wasafirishaji rasmi (Official Carriers) kama njia ya kusaidia na kuinua michezo
nchini,” alisema Mkurugenzi huyo ambaye pia alishiriki katika mbio hizo. “Ila lazima tuongeze
munkari ya kujifunza, kukuza vipaji toka udogoni, na viongozi wa michezo wetu
waweze kujitahidi kuwatafutia wachezaji wetu nafasi za kung’ara, huku sisi
wadhamini pia tukitumia nafasi zetu kwa kuendelea kutoa sapoti,” alisema.
Kwa upande mwingine
Ndekana alitoa pia wito kwa watanzania kujenga desturi ya kutembelea vivutio
vya utalii ikiwemo Mlima Kilimanjaro na mbuga mbali mbali za wanyama zilizopo
nchini.
Akizungumzia umuhimu
huo Bw Ndekana alisema, “Nchi yetu Tanzania ina vivutio na rasilimali nyingi
sana, ikiwemo huu mlima maarufu….ingekuwa vizuri kwa sisi pamoja na watoto wetu
na vizazi vijavyo kuja na kuweza kujifunza asili yetu kwa kutembelea haya maeno
kuliko kuishia kuona tu katika luninga au kusoma katika vitabu.”
“Lakini pamoja na hayo
hii itakuwa fursa nzuri pia kuchangia katika pato letu la taifa na kuzidi
kuinua sekta yetu ya utalii nchini,” alisema Ndekana. Bw. Ndekana pia aliwakaribisha umma kusafiri na
shirika hilo la ndege kuweza kutembelea vivutio vya utalii mbali mbali nchini
kwa sababu shirika hilo linasafiri karibu kila kona ya nchi ikiwemo sehemu kama
Kilimanjaro, Mwanza, Zanzibar na kadhalika huku akisisitizia kuwaptia huduma
bora kwa wasafiri wake.
Hii
ni mara ya pili sasa kwa Precision Air kudhamini mashindano ya Kilimanjaro
Marathon yanayofanyika kila mwaka Moshi, Kilimajaro. Shirika hilo ina mtandao mkubwa nchini kuliko mashirika yote
Tanzania, ikiwa inafanya safari kwenda;
Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Bukoba, Kigoma,
Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara. Kikanda Precision Air inasafiri kwenda Nairobi, Mombasa, Entebbe, Hahaya na
Johannesburg.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)