MAN U YAICHAPA LIVERPOOL 2-1 NA KUKAA KILELENI - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Breaking

Home Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

MAN U YAICHAPA LIVERPOOL 2-1 NA KUKAA KILELENI

 Mshambuliaji wa timu ya Manchester United,Wayne Rooney (wapili kushoto) akifunga bao la kwanza katikati ya mabeki wa Liverpoo,Daniel Agger(kulia) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Old Trafford, Manchester.

Man U imeshinda mabao 2-1 na kuipiku Man City kwa Pointi 1, ambapo kwa sasa Man U inaongoza ligi hiyo ikiwa na jumla ya Pointi 58, ikifuatiwa na Man City yenye Pointi 57, Tottenham inafuatia ikiwa na Pointi 50, Chelsea inashika nafasi ya nne, ikiwa na Pointi 43, huku ikifutiwa na Newcastle yenye pointi 42, Arsenal ikiwa na Pointi 40 na Liverpool ikiwa nafasi ya saba na ikiwa na Pointi 39. Baadhi ya timu mbali na Liverpool pointi hizo ni kabla ya michezo yao ya leo. 

 Rooney akishangilia bao lake.....
 ''WE HAPA HUPITI NITUKANE TENA URUDI JELA''
Beki wa Man U, Patrice Evra  (wa pili kushoto) akimdhibiti mbaya wake, Luiz Suarez, wakati wa mchezo huo
.
 Mshambuliaji wa Liverpool, Luiz Suarez (kulia) akichuana kuwania mpira na kiungo wa Man U, Michael Carrick, wakati wa mchezo huo.
 Rafael Da Silva (juu) akikwepa kwanja la kiungo wa Liverpool, Stewart Downing, wakati wa mchezo huo.
 Danish defender wa Liverpool (kulia) akichuana na Danny Welbeck wa Man U.
 Antonio Valencia wa Man U (kulia) akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Liverpool, Jay Spearing.
 Mahasimu wawili beki wa Man U, Patrice Evra na mshambuliaji wa Liverpool, Luiz Suarez, wakisalimiana na kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Ni kama wanaliana timing ya kuombana msamaha

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here

Pages