MAKAMU
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa
kilele cha maadhimisho ya sherehe za kuzaliwa Chama Cha mapinduzi CCM,
kimkoa zinazotarajia kufanyika Februari 5, mwaka huu zitakazofanyika
mlandizi wilayani Kibaha mkoani Pwani.
Hayo
yamesemwa na katibu wa CCM mkoa wa Pwani, Sauda Mpambalyoto, wakati
akitoa taarifa ya kazi za chama na jumuiya zake baada ya Makamu, kukagua
ukarabati wa jengo la CCM wilaya ya RUfiji ambalo litakuwa na ofisi za
Chama na jumuiya zake mjini Utete wilayani Rufiji.
Amesema
maadhimisho hayo ni sehemu ya utaratibu wa kimkoa kwenda kila wilaya
kusheherekea maadhimisho hayo ilikuhamasisha kwa kuwafuata wanachama
kila wilaya na kuwajali kuwa ni sehemu ya chama chao.
Mpambalyoto,
amesema katika maadhimisho hayo ataongoza matembezi ya mshikamano kwa
kilo mita tano ambapo mwaka huu matembezi hayo ni kumdhamini Mwenyekiti
wa CCM Taifa Dkt. JAKAYA KIKWETE na baadaye kwenda kuyapokea katika
viwanja vya shule ya msingi Mtongani Mlandizi ambayo yataanzia katika
ofisi ya chama wilaya.
Amesema
pamoja na mambo mengine atapokea wanachama wapya zaidi ya 2000 kutoka
chama na jumuiya zake kutoka mkoa mzima wa Pwani na kutoa hati kwa
wilaya kwa wilaya zilizofanya vizuri katika uingizaji wa wanachama kwa
chama na jumuiya zake, wilaya zilizokusanya ada vizuri kwa chama na
jumuiya zake, wilaya zilizofanya vikao vya chama na jumuiya zake kwa
wakati ambapo hati hizo zitatolewa kwa mshindi wa kwanza hadi wa tatu
pia atatoa hati zilizokusanya fedha nyingi kwa matembezi ya mshikamano
mwaka 2011.
Aidha
amefafanua kuwa maadhimisho hayo yatahudhuriwa na viongozi wote na
wanachama kutoka wilaya zote na wilaya ya kibaha kwa kuwa ndio wenyeji
wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika kumpokea mgeni huyo ambaye ni
mlezi wa CCM mkoa na mjumbe wa kamati mkuu na halmashauri kuu ya CCM na
makamu wa Rais wa jamuuhuri ya muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)