Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Mkazi wa Kijiji cha Mwamapuli, Yacoub Jilala, ambaye ni
mlemavu, baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa kijiji hicho,
alipofika kuzindua jengo la Ghara la mazao, akiwa katika ziara yake ya
mkoa wa Rukwa na Katavi, juzi Februari 20, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la
Msingi katika jengo la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya
Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake
ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kushoto kwake ni
mkewe Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe
kuzindua rasmi jengo la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya
Korongwe Beach , iliyopo Wilaya ya Nkasi, wakati akiwa katika ziara yake
ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012. Kulia kwake ni
mkewe Mama Asha Bilal.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akinawa maji ya Kisima cha kupampu yanayovunwa kwa mvua,
kilichojengwa katika Kijiji cha Mwamapuli wakati alipokuwa katika ziara
yake ya mkoa wa Rukwa na Katavi juzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda Mti wa kumbukumbu nje ya jengo
la Daharia la Shule ya Sekondari ya wasichana ya Korongwe Beach ,
iliyopo Wilaya ya Nkasi, baada ya kuzindua Daharia hilo wakati akiwa
katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi, jana Februari 21, 2012.
Nyuma yake ni mkewe Mama Asha Bilal na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Eng. Stella Manyanya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwasili kwenye Uwanja wa Korongwe kwa ajili ya kuwahutubia wananchi
wakati akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Rukwa na Katavi jana Februari
21, 2012.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)