Meneja
Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minja walioidhamini timu ya
Riadha ya Mkoa wa Arusha katika Mbio za Kilimanjaro Marathon 2012,
akiwapa mkono wa heri na kuwatakia ushindi wanariadha hao 18,
wanaouwakilisha mkoa wa Arusha katika mbio hizo zitakazofanyika kesho
mjini Moshi, mkoani Kilimnajaro. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha
Riadha Mkoa wa Arusha ambaye pia ni kocha wa riadha wa timu hiyo, John
Bayo.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha ambaye pia ni kocha wa riadha
wa timu ya mkoa wa Arusha, John Bayo (kushoto) akizungumza jambo na
wanariadha wanaouwakilisha mkoa wa Arusha katika Mashindano ya mwaka huu
ya Kilimanjaro Marathon yatakayofanyika kesho mjini Moshi. Kulia ni
Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minja walioidhamini timu
hiyo kushiriki mashindano hayo.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minja walioidhamini timu ya
Riadha ya Mkoa wa Arusha katika Mbio za Kilimanjaro Marathon 2012, akiwa
katika picha ya pamoja na makocha wanaoinoa timu ya mkoa wa Arusha.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya CFAO Motors, Alfred Minja walioidhamini timu ya
Riadha ya Mkoa wa Arusha katika Mbio za Kilimanjaro Marathon 2012, akiwa
katika picha ya pamoja na wanariadha.
Wachezaji
wa timu ya Riadha ya mkoa wa Arusha inayoshiriki mashindano ya
Kilimanjaroo Marathon 2012 wakijiandikisha kushiriki mashinado hayo jana
tayari kwa mashindano hayo makubwa yatakayofanyikia kesho mjini Moshi
mkoani Kilimajaro. Timu hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors ya
jijini Dar es Salaam na inajumla ya wakimbiaji 18.
Wachezaji
wa timu ya Riadha ya mkoa wa Arusha inayoshiriki mashindano ya
Kilimanjaroo Marathon 2012 wakijiandikisha kushiriki mashinado hayo jana
tayari kwa mashindano hayo makubwa yatakayofanyikia kesho mjini Moshi
mkoani Kilimajaro. Timu hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors ya
jijini Dar es Salaam na inajumla ya wakimbiaji 18.Picha Zote na Mpiga
Picha Wetu
----
Na Mroki Mroki,Moshi
TIMU
ya riadha kutoka Mkoa wa Arusha, imejigamba kuibuka na ushindi mnono
katika Mshindano ya mwaka huu ya mbiuo za nyika yajulikanayo kama
Kilimanjaro Marathon 2012 yatakayofanyika kesho mjini Moshi mkoani
Kilimanjaro.
Timu
hiyo ambayo, imedhaminiwa na Kampuni ya CFAO Motors ya jijini Dar es
Salaam imesema mwaka huu haipo tayari kuachia medali za dhahabu, Shaba
na fedha ziende nchini Kenya na badala yake watahakikisha kuwa zinabaki
hapa nchini.
“Tumejipanga
vizuri sana mwaka huu na wachezaji wetu wote waliingia kambini kujifua
vizuri chini ya udhamini mzuri wa CFAO Motors, hivyo watanzania wake
tayari kushangilia ushindi”,alisema Kocha wa timu hiyo ambaye pia ni
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha,John Bayo.
Aidha
Bayo alisema timu ya Arusha inaundwa na wachezaji mashuhuri na walio na
rekodi nzuri za mashindano hayo nay ale ya kimataifa.
Aliwataja
wachezaji wanounda timu hiyo ya Arusha iliyo na wakimbiaji 18 kuwa ni
Fabiola William, Banuuelia Katesigwa, Flora Kagali, Rebeca Kavina, Daudi
Joseph, Mashaka Masumbo, Yohana Masuka na Josepha Elias ambao hukimbia
Full Marathon.
Wengine
watakao kimbia Nusu marathon (21km) ni Mary Naali, Fabian Joseph,
Faustine Mussa, Ezekiel Jfari, Uwezo Lukinga, Rogart John, Joseph
Francis, Restituta Joseph, Jacquline Sakilu na Damian Chopa.
Nae
Meneja Masoko wa Kampuni ya CFAO iliyodhamini timu hiyo ya mkoa wa
Arusha, Alfred Minja, amesema kampuni yake imetumia Shilingi milioni 35
katika mashiondano ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na kudhamini timu hiyo
na uratimu waa mashindano.
Minja
alisema mwaka wa 10 sasa CFAO Motors inadhamini mashindano ya
Kilimanjaro Marathon na mwaka 4 sasa kudhamini timu ambazo zimekuwa
zikifanya vizuri.
Aidha
amesema CFAO Motors itakuwa na meza maalum ya kugawa maji, soda,
vitafunwa na burudani ya muziki kwa katika eneo la Mweka ambapo
wakimbiaji watakuwa wakigeuzia.
Minja
amesema CFAO Motors, mbali na kudhamini wachezaji hao wa timu ya Arusha
18 lakini pia inawakimbiaji wengine 25 wa nusu marathon kutoka jijini
Dar es Salaam.
Mashindano
ya Mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon yanataraji kuwa na shamra shamra
za aina yake Ambato pia yatakiwa yanatimiza mwaka wa kumi tangu kuanza
kufanyika.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)