Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika hatua mbalimbali za kusaidia kufyatua
matofali ya kisasa kwenye kambi ya mafunzo ya ujasiriamali na ujenzi kwa
vijana 380 toka wilaya zote za Mkoa wa Pwani za Kibaha mjini Kibaha
vijijini, Mafia, Kisarawe, Mkuranga na Rufiji.

Kambi hiyo ya mwezi mmoja iliyo katika kijiji cha Msoga, wilaya ya
Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, ni moja kati ya kambi kadhaa zinazoandaliwa
mkoani humo, ambapo ikimalizika hii ya ujenzi mnamo february 29,
itafuatia ya upandaji miti na mazingira itakayokuwa katika Chuo cha
Elimu Kibaha. Baada ya Hapo itafuatiwa kambi ya ukulima wa mazao ya
mbogamboga wilayani Rufiji.
Rais Kikwete ameusifu mkoa wa Pwani kwa kubuni kambi
hizo na kutaka mikoa mingine iige mfano huo ili kuwapa vijana ujuzi wa
kuweza kujiajiri wenyewe.
Ameahidi kuendelea
kusaidi vikundi vya vijana vya aina hiyo ambavyo amevitaja kama hazina
nzuri ya maendeleo na utatuzi wa vitendo wa tatizo la ajira.
Rais Kikwete ametoa mashine za kufyatulia matofali
ya kisasa 76 ambapo kila moja kati ya vikundi 38 vilivyopo vitapewa
mashine mbili mpya na waliyofanyia kazi wataondoka nayo na kuwa ya tatu.
Pia Amewapa vijana hao mifuko 3800 ya saruji (kila kundi mifuko 100),
viatu vigumu (gum boots) pamoja na mananasi toka shambani kwake. PICHA NA HABARI NA IKULU
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)