Afisa Uhusiano katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Aminieli Eligaesha akizungumza
na waandishi wa habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam (hawapo
pichani) kuhusu kurejea kwa huduma za afya katika hospitali hiyo,
kufuatia mgomo wa madaktari bingwa na wauguzi uliofanywa katika kipindi cha wiki tatu sasa.
Muuguzi
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akipitia jalada kabla ya kwenda
kutoa matibabu kwa mgonjwa katika wodi ya Kibasila ya Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili leo.
Daktari
Charles Some wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akimtoa damu kwa ajili
ya vipimo vya matibabu kwa Bi. Upendo Msangi katika wodi ya kibasila.
Madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo wamerejea kazini leo (jana)
kufuatia agizo lililotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana (juzi) la kuwataka kurejea katika maeneo yao ya kazi.
Baadhi
ya wananchi wakiwa katika hospitali ya amana, wakisubiri huduma za
matibabu katika hosptali hiyo, kufuatia kurejea kazini kwa madaktari na
wauguzi katika hospitali hiyo mara baada ya mgomo uliodumu katika kipindi cha wiki tatu sasa.
Muuguzi
wa kubeba wagonjwa katika hospitali ya Amana Ilala, Mohamed Ally
akimpeleka katika chumba wagonjwa, Bi Domitila Haule tayari kupatiwa
huduma za matibabu katika hospitali hiyo. Madaktari na wauguzi wamerejea
kazini leo kufuatia mgomo waliouitisha takribani wiki tatu sasa.Picha Na John Bukuku Wa Full Shangwe
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)