Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud Mohamed
akitoa taarifa kuhusu kilele cha Sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi
Zanzibar mbele ya waandishi wa habari huko Ofisi kwake Vuga Mjini
Zanzibar.Picha zote na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar
--
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Zaidi
ya Shs. Million 700 zinatarajiwa kutumika katika kuadhimisha Sherehe za
miaka 48 ya Mapinduzi Zanzibar ambayo kilele chake kitakuwa Januari 12
Mwezi huu huko katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar
Akitoa
taarifa mbele ya waandishi wa habari leo huko ofisini kwake Vuga,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed
amesema kuwa fedha hizo ni kwa makisio tu lakini taarifa kamili ya
matumizi hayo itatolewa baada ya kukamilika kwa sherehe hiyo
Amesema
kuwa sherehe za mwaka huu zitakuwa ni tofauti kidogo tu ukilinganisha
na miaka iliyopita kwani wanafunzi hawatoshirikishwa wakiwa wamevaa sare
zao kwani imeonekana kuwa wananchi wengi watahudhuria sherehe hizo.
Amesema
kuwa Kiwanja kilichokuwepo kwa sasa hakikidhi haja ya kuweza kuwachukua
wananchi wanaokadiriwa kuzidi uwezo wa uwanja huo ambao ni watu 15 Elfu
tu.
Hata
hivyo Waziri Aboud amesema kuwa Wanafunzi hawakatazwi kuja kusherehekea
wakiwa wamevaliwa nguo zao kama wananchi wa kawaida
Akizungumzia
suala la Sherehe hizo kuitwa za Mapinduzi wakati Zanzibar inaendesha
Chaguzi zake kwa njia za kidemokrasia, amesema kuwa Neno Mapinduzi ni
kitu ambacho kilichowagomboa wananchi wa Zanzibar kwa hivyo Serikali
imeona iko haja ya neno hilo lienziwe kwani Mapinduzi ndiyo
yaliyowagomboa Wananchi wa Zanzibar kutoka katika makucha ya Wakoloni.
Aidha
amewapongeza wananchi wa Zanzibar pamoja na waandishi wa habari kwa
mashirikiano yao makubwa ambayo wameyaonesha katika kusherehekea sherehe
hizo za miaka 48 ya Mapinduzi tangu kuanza kwake tarehe 4 mwezi huu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)