
Mkuu
wa kitengo cha mauzo ya Vodacom m-pesa Franklin Bagala,akiongea na
Mawakala wa m-pesa wa Mkoa wa Dares Salaam katika semina iliyoandaliwa
na Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala hao kujifunza namna ya kutoa
huduma zilizo bora za m-pesa kwa wateja wao,Semina hiyo ilifanyika kwa
siku mbili katika ukumbi wa Karimjee jijini.
********************************
********************************
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mtandao Vodacom m-pesa waboreshwa
· Kasi yaongezeka. Wateja wazidi kufurahia huduma.
Dar es salaam Disemba 15, 2012.
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imefanya maboresho makubwa
katika mfumo unaondesha huduma ya Vodacom m-pesa kwa lengo la kuendana
na kasi ya ukuaji na mahitaji ya huduma hiyo katika soko nchini.
Maboresho hayo sasa yanawawezesha wateja wa Vodacom m-pesa kufanya miamala yao kwa ubora na kasi ya hali ya juu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza amesema maboresho hayo
makubwa yamefanyika Disemba mwaka jana ili kuuongeza nguvu na ufanisi
mfumo wa mawasiliano unaotumika kutoa huduma za Vodacom m-pesa.
“Tumefanya
maboresho kama ilivyodesturi yetu ya kuboresha na kuimarisha huduma
zetu mara kwa mara. Tunatambua kwamba wateja wa Vodacom m-pesa walikuwa
wanakabiliwa na changamoto za hapa na pale ninayo furaha kubwa kuona
kwamba tunaendelea kuiboresha huduma hii”Alisema Bw. MezaBw. Meza
amesema katika kipindi chote cha mwishoni mwa mwaka huduma ya m-pesa
imepatikana kwa kasi na ubora zaidi na hivyo huduma ya m-pesa kuendelea
kuwa kiungo muhimu katika kubadili maisha ya wananchi kupitia teknolojia
ya simu ya mkononi.
“Wakati
wote tunaishi na dhamira yetu ya kutoa huduma bora na kujali mahitaji
ya wateja wetu tutaendelea kufanya hivyo mara kwa mara sambamba na kutoa
kipaumbele cha kuhakikisha usalama huku tukiongeza pia kasi ya ubunifu
na uvumbuzi wa huduma bora”. Alisema Bw. Meza.
“Huduma
ya Vodacom m-pesa imekuwa kiungo muhimu cha maisha ya wananchi mijini
na vijijini imezalisha ajira, imerahisisha maisha na biashara ni kiasi
cha kupiga *150#00 kutoka mtandao wa Vodacom na kuanzia hapo
kiganja cha mkono kinakusogeza karibu na ndugu jamaa na watoa huduma
mbalimbali.” Bw.Meza aliongeza.
Huduma
ya Vodacom m-pesa imeanzishwa Aprili 2007 na tangu wakati huo ukuaji
wake sokoni umekuwa ni wa kasi kufikia wateja milioni tisa kutokana na
kutoa urahisi wa malipo na ununuzi wa huduma mbalimbali ikiwemo
Maji,Umeme, muda wa maongezi, Dstv, manunuzi ya tiketi za safari za
ndege, utumaji na upokeaji wa fedha kwa usalama,uhakika na kuaminika
wakati wote ukiwa na mtandao wa wakala zaidi ya elfu ishirini nchi
nzima.

Mmoja
wa mawakala wa mkoa wa Dares Salaam akiinua mkono kuuliza swala katika
semina ya mawakala wa m-pesa wa mkoa wa Dares Salaam iliyoandaliwa na
Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala hao kwa ajili ya kutoa huduma
bora za m-pesa kwa wateja wao,Semina hiyo ilifanyika kwa siku mbili
katika ukumbi wa Karimjee jijini.

.
Baadhi ya Mawakala wa m-pesa wa Mkoa wa Dares Salaam waliohudhuria
katika semina iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania,mahususi kwa mawakala
hao kujifunza namna ya kutoa huduma bora za m-pesa kwa wateja
wao,Semina hiyo ilifanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa Karimjee
jijini.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)