Waziri
wa Ujenzi Dakt. John Pombe Magufuli (katikati) akisisitiza jambo
wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Jan,
1,2012 kuhusu ongezeko la viwango vya nauli katika vivuko vyote vya
serikali nchini, ambapo kuanzia Jan, 1 ,2012, Wizara yake kupitia
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imeongeza viwango vya nauli kutokana
na maeneo mbalimbali ya vivuko, , amezitaja nauli hizo kwa mfano
MV. Magogoni na Mv. Kigamboni kwa Mkoa wa DSM ni kati ya shilingi 200
kwa watu wazima , watoto chini ya miaka 14, shilingi 50, na wanafunzi
waliovaa sare za shule na vitambul;isho ni bure, Pia akatoa mfano wa
Kivuko cha MV. Chato kitatoza nauli ya watu wazima shilingi 3,000/,
watoto chini ya miaka 14 ni elf 50 ,na wanafunzi wenye sare za shule
ni bure. Bei hizi zimepanda kutokana na gharama kupanda za uendesaji.
(kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA Prof, Idrissa Mshoro. (kushoto)
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Herbert Mrango.
-Waziri
wa Ujenzi Dk. John Magufuli (kushoto) akiongea na waandishi wa habari
hawapo pichani Jan, I, 2011 jijini Dar es Salaam kuhusu ongezeko la
viwango vya nauli katika vivuko. Wizara ya Ujenzi kuanzia tarehe 1
Januari kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imeongeza viwango
vya nauli katika vivuko vyote vya serikali nchini, (kulia) ni
Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA Profesa Idrissa Mshoro
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Balozi Herbert Mrango (kushoto)
akimkaribisha Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (katikati)
alipokutana na waandishi wa habari hawapo pichani jijini leo na kutoa
taarifa kuhusu ongezeko la viwango mbalimbali vya nauli katika vivuko
nchini , (kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEMESA Prof, Idrissa Mshoro,
(Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)