Mgeni rasmi wa hafla hiyo,Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba
pichani kati,shoto kwake ni Mkurugenzi wa huduma za uuguzi hospitali
ya Taifa Muhimbili na mwisho kabisa ni Mwendesha kipindi cha Njia
Panda,Dr Isaac Maro wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wengine wa
kipindi hicho kinachorushwa na Clouds FM kila siku ya jumapili..
Jamii,Jinsia
na Watoto,Mh Sofia Simba akizungumza na baadhi ya wazazi wanaowauguza
watoto wao kwenye Wodi ya Watoto wenye matatizo ya saratani
wanaotibiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili,kabla ya kutoa msaada
kwenye wodi hiyo iliyotolewa na Wadau mbalimbali wa kipindi cha Njia
Panda kinachoongozwa na Dr Isaac Maro kupitia redio ya Clouds FM kila
siku ya jumapili,pichani nyuma ni baadhi ya Wadau wa kipindi cha Njia
Panda ambao walifika kwenye Wodi hiyo sambamba na kuwapa pole watoto
wanaosumbuliwa na saratani,hafla hiyo fupi imefanyika leo jijini Dar.
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba akimlisha keki
mtoto anayelelewa na kipindi cha Njia Panda,dada Juliana
Maganyiro,ambaye leo ni siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka
19,ambapo yeye na wadau wengine wa Njia Panda waliamua kufanya hafla
fupi sambamba na kutoa msaada katika wodi ya watoto wenye matatizo ya
saratani.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo,Waziri
wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba akimkabidhi
sehemu ya msaada uliotolewa na kipindi cha Njia Panda,kwa niaba ya
Mganga Mkuu,Mkurugenzi wa huduma za uuguzi hospitali ya Taifa
Muhimbili,Dada Agnes Mtawa.
Waziri
wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba akizungumza na
Mama anayemuuguza mtoto wake mwenye matatizo ya saratani na kumpa
pole,Pichani kati ni mtoto anayelelewa na kipindi cha Njia panda aitwaye
Juliana Maganyiro ambaye ni mtoto yatima aliyeamua kula keki yake ya
sherehe ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 19 tangu kuzaliwa kwake na watoto
walioko kwenye wodi hiyo.
Leo
hii kipindi cha Njia Panda kimefanya hafla fupi ya mwaka mpya katika
wodi ya watoto wenye matatizo ya saratani,wanaotibiwa katika hospitali
ya Taifa Muhimbili,hafla hiyo iliambatana na sherehe fupi ya siku ya
kuzaliwa ya mtoto Juliana Maganyiro ambaye amekuwa akilelewa na kipindi
cha Njia Panda tangu alivyokuwa na umri wa miaka 13,Juliana ni mtoto
Yatima na amekuwa chini ya Kipindi cha Njia Panda kwa miaka 6
sasa,aidha katika hafla hiyo iliyofanyika leo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri
wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto,Mh Sofia Simba.Pichani mbele
kulia ni Dada Juliana na nyuma kabisa ni mwendeshaji wa kipindi cha
Njia Panda,Dr Isaac Maro akiwa na Mwanaharakati mwingine wa kipindi
hicho Bw.Edmond Lyatuu.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)