Vijana wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu
ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina,
kabla ya mwili huo kusafirishwa leo kwenda Korogwe kwa mazishi.
Shughuli hiyo ilifanyika nyumbani kwa marehemu, Wazo, Dar es Salaam.
Makamu
Mkt wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Mukama na Nape wakizungumza na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omari Chambo wakati wa shughuli ya kuaga
mwili wa marehemu Balozi Mhina, Wazo, Dar es Salaam, leo.
Wasira
akijadili jambo na Nape kwenye shughuli hiyo ya kusafirisha mwili wa
marehemu Balozi Mhina leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha CCM,
Mwigulu Nchemba.
Katibu
Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani
kwa Balozi Mhina, Wazo kabla ya kusafirisha mwili kwenda Korogwe,
Tanga, leo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akisaini kitabu cha
maombolezo nyumbani kwa Balozi Mhina, kabla ya mwili kusafirishwa
kwenda Korogwe, leo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Mukama akimfariji, Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi
(Zanzibar) Dogo Mabrouk wakati wa shughuli za kusafirisha mwili wa
aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuia hiyio Balozi Mhina, leo.
Wanafamilia wakiwa katika majozi wakati wa shughuli ya kusaifirishwa mwili wa marehemu leo.(Picha na Bashir Mkoromo)
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)