Wafanyakzi
wa Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania, wanaotoa huduma mbalimbali
katika kambi za waathirika wa mafuriko jijini Dar es Salaam wakiandaa
ugali wa mchana hii leo katika eneo la Mabwe Pande nje Kidogo ya jiji la
Dar es Salaam ambako baadhi ya waathirika hao wanaandaliwa viwanja na
makazi ya muda.
hapa ni ugali unaonjwa kama upo tayari kwa kuliwa.
kazi
kubwa wanayo ifanya Msalaba Mwekundi hapo Mabwe pande hivi sasa ni
kujenga makazi ya Muda ambayo waathirika wa mafuriko hasa wale waliokuwa
na nyumba mabondeni watahamia.
mahema yaliyo kamilika yaliwekwa nembo maalum za Shirika hilo.
Mslaba Mwenkendu imetoa mahema zaidi ya 200 katika eneo hilo ambayo tayari yamefungwa.
Hakika
eneo hili litakuwa zuri na lililo katika mpangilio mzuri sana pindi
wahusika wakifika na kujenga makazi yao ya kudumu. Seruikali imeahidi
kusogeza huduma zote muhimu kama maji, Umeme na vituo vya afya katika
eneo hilo. Lakini watu wanahofu juu ya waliokuwa wamiliki wa nyumba hizo
za jangwani na bonde la Msimbazi kuwa kama wataenda kuishi huko. Ama
watauza viwanja hivyo? Picha Na Father Kidevu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)