Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua
jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto baada ya kuweka jiwe la Msingi katika
jengo hilo
lililopo Chakechake Lushoto jana Januari 27, 2012, wakati akiwa katika ziara
yake ya mkoa wa Tanga. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa na
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Sophia Mjema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasalimia na kuwaaga wasanii waliokuwa wakitoa
burudani, wakati akiondoka Chakechake baada ya kuweka jiwe la Msingi katika
Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, jana Januari 27, 2012, wakati akiwa
katika ziara yake ya mkoa wa Tanga
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia
chupa ya Juisi iliyotengenezwa na wajasiliamali, Salome Mtawa (kulia) wa
kikundi cha Usambara Lishe Trust, wakati
alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha
Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa
Tanga
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkulima wa Nyanya, Judith
Munis, wa Kikundi cha Upendo Jegestal, kuhusu kilimo cha nyanya, wakati
alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha
Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)