Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa
Kichina, zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini
(CBCT), zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
Salaam jana jioni Januari 15.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 16, kutoka kwa
Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na
City Bank Tanzania LTD kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko
yaliyotokea jijini Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana,
ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina
zilizofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari
15.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea mfano wa Hundi, yenye thamani ya Sh. Milioni 10, kutoka kwa
Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, (kulia) iliyotolewa na
Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina wa Tanzania (CBCT) kwa ajili ya
kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka jana, ikiwa ni sehemu ya sherehe za
kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika kwenye Viwanja vya
Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana Januari 15.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng ,
wakati alipohudhuria sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina,
zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini (CBCT),
zilizofanyika jana jioni Januari 15, kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya wasanii wa Kichina waliokuwa wakitoa burudani
jukwaani wakati wa sherehe hizo, wakati akijiandaa kuondoka katika
Viwanja hivyo.
Makamu
Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongoza na Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng, wakati
akiwasili kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jinni Dar es Salaam jana jioni
Januari 15, katika sherehe za kuukaribisha mwaka mpya wa Kichina,
sherehe zilizoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa Kichina nchini
(CBCT)Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)