Majina ya Walioteuliwa Kushiriki Kozi ya Ngumi Yatajwa - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Majina ya Walioteuliwa Kushiriki Kozi ya Ngumi Yatajwa


Kocha wa mchezo wa ngumi wa timu ya Ashanti na timu ya Mkoa wa Ilala kimichezo. Rajabu Mhamila 'Super D' Pichani  ameteuliwa kushiriki katika kozi hiyo ya kimataifa
---
Na Mwandishi Wetu
 SHIRIKISHO la Ngumi za ridhaa nchini (BFT) limepiga panga majina matano kati ya 30 ya makocha walioteuliwa kushiriki katika kozi ya kimataifa ya mchezo huo iliyopangwa kufannyika Januari 16 mwaka huu.

BFT imewakata washiriki hao baada ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki kutokana na hasara iliyosababishwa na washiriki hao katika kozi ya awali iliyokuwa  ifanyike tangu mwezi Novemba mwaka jana.

TOC ambayo huandaa kozi za michezo mbalimbali kutokana na ruzuku inayotolewa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ilikuwa iendeshe kozi hiyo tangu mwaka jana lakini haikufanyika kutokana na mkufunzi wa kozi hiyo kutoka nchini Algeria kuingia mitini.

TOC ililazimika kuwalipa nauli baadhi ya washiriki waliotoka nje ya Dar es Salaa kutoka katika fungu la pesa   za kuendeshea kozi hiyo hivyo kuwataka BFT kupunguza idadi ya washiriki hasa wale waliofanya utovu wa nidhamu katika kozi ya awali ili kiwango cha pesa kilichobaki kutosheleza mahitaji wa kozi  itakayoendeshwa Januari 16 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam Katibu mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema idadi ya makocha 25 waliowateua inaweza ikapungua tena kulingana na
bajeti waliobaki nayo TOC ambapo hata hivyo hakuyataja majina matano
ya washiriki walioachwa .

Aliwataja washiriki waliopenya kuhudhuria kozi hiyo ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na Jarida la Maishaambaye pia alikuwa bondia, Rajabu Mhamila 'Super D', Anord Ngumbi, Moses Lema,Anthon Mwang'onda na Edward Emanuel (Dar es Salaam).

Wengine ni Yahaya Mvuvi (Tabora), Joseph Mayanga na Zakaria Mwaseba(Morogoro), Omari Saady na Mussa Bakari (Mwanza), Ally Ndee (JKT Mbeya), Emilio Moyo na Gaudens Uyaga (Pwani) Juma Liso (MagerezaKigoma), Lyinda Kalinga (Dodoma) na Abdalah Bakari  (Tanga).

Wengine ni  Mohamed Hashim  (Polisi Dar es Salaam), David Yombayombam, Haji Abdalah, Said Omari (JWTZ),  Mazimbo Ally, Rogated Damian na Fatuma Milanzi (JKT), Musa Maisori na Hamisi Shaaban (Magereza Dar es Salaam).

Kozi hiyo itaendeshwa na mkufunzi wa kimataifa Josef Diouf kutoka Shirikisho la Dunia la mchezo huo (AIBA) ambaye atashirikiana na makamu wa Rais wa BFT, Michael Changarawe.
Kozi hiyo itafanyika  latika shule ya Sekondari ya Filbert Bayi Kibaha Mkoani Pwani  na itafikia tamati  Januari 24 mwaka huu.

Mwisho

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages