Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa
awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman
mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za
maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa
Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman
mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za
maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiwa jukwaani Uwanja wa Amani katika Sherehe hizo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri, Mama
Zakhia Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, wakiwa katika sherehe hizo.
Kutoka (kulia) Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad,
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri, Mama Asha Bilal,Rais Mstaafu wa awamu
ya tatu, Benjamin Mkapa, Jaji Mkuu, Othman Chande na Rais Mstaafu wa
Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakiwa katika sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Wawakilishi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwa jukwaani wakati
ukipigwa wimbo maalum wa Taifa wa Zanzibar
Wanajeshi wa Jeshi la wananchi la Tanzania Wakionyesha Ujuzi wao mbele ya Jukwaa kuu
Kikosi cha Wanajeshi waenda kwa miguu, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni wa rasmi.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein,
akikagua gwaride maalum wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 48 ya
Mapinduzi ya Zanzibar
Kikosi cha kutuliza ghasia FFU, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa Mgeni rasmi.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)